Loading...

DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA.

Loading...
DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA. - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA.
link : DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA.

soma pia


DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA.

NA TIGANYA VINCENT
RS-TABORA
SERIKALI ya Mkoa wa Tabora imewataka watendaji wote katika ngazi mbalimbali kuacha kukaa ofisini badala yake washirikiane na wakulima ili waweze kuwa na  uzalishaji utakao wapatia tija na hivyo kuondokana na umaskini.
Kauli hiyo jana na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Rehema Nchimbi wakati akikagua mashamba mbalimbali ya pamba ili kujionea zoezi la unyunyuziaji wa viua wadudu wilayani Igunga.
Alisema kila mtumishi kwa nafsi yake bila kujali cheo na kazi yake ni lazima hakikishe anafanyakazi kwa ajili kuwasaidia wakulima kuzalisha mazao mengi ambayo yatakayowasaidia kujiendeleza wenyewe na taifa kwa ujumla.
Dkt. Nchimbi alisema nguvu za watumishi ni vema zikaelekezwa katika kutatua vikwazo mbalimbali ambavyo vinawakwamisha wakulima wasiweze kufanya vizuri katika kilimo chao.
“Wakulima wetu ni wasikivu sana lakini wamekuwa wakikosa ushauri kutoka kwa wataalamu na kwetu sisi ndio maana unaona kuwa wamekuwa wakichelewa kunyunyuzia dawa za kuua wadudu” alisema Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa.
“Tutoke Maofisini na twende kwa wakulima kuwasaidia…ukiwa mtumishi wa umma ni lazima ujue vitu vingi ambavyo vitasaidia wakulima…usiseme mimi ni Mtendaji wa Kijiji suala la kilimo ni la Afisa Ugani, pekee utakuwa unakosea ni lazima tufanye kazi kama timu ya mpira inavyokuwa uwanjani ili wakulima wakifanya vizuri basi tuonekane wote tumefanya vizuri na wakifanya vibaya basi lawama ziwe kwetu wote” alisema Dkt. Nchimbi.
Kaimu Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora aliongeza kuwa wakulima wamekuwa wakipata hasara kwa sababu ya kukosa ushauri kutoka kwa wataaalamu au watendaji ambao ungeweza kuzuia uharibifu katika mazao yao.
Alisema kuwa Serikali iliyopo madarakani inawataka watumishi wote kuwa msaada wa wakulima katika shughuli zao ili waweze kuzalishaji kwa wingi kwa ajili ya kupata bidhaa zitakazosaidi ujenzi wa uchumi wa viwanda.
Dkt. Nchimbi amemaliza ziara ya siku tatu wilayani Igunga ambapo alitembelea mashamba mbalimbali ya wakulima na kutoa elimu ya unyunyuziaji wa viua wadudu katika zao la pamba.


Hivyo makala DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA.

yaani makala yote DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/dktnchimbi-ondokeni-maofisini-nendeni.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DKT.NCHIMBI : ONDOKENI MAOFISINI NENDENI MKAWASAIDIE WAKULIMA."

Post a Comment

Loading...