Loading...
title : Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi
link : Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi
Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi
Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi.
Serikali ya Tanzania imeweka mkazo kuboresha mazingira ya elimu kwa wanafunzi katika kujifunza ambayo ndiyo chachu ya mabadiliko na kufanya sekta hiyo nyeti ipige hatua.
Miongoni mwa mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na ongezeko la uandikishaji, kuleta usawa wa kijinsia kwenye shule za msingi na sekondari nchini.Kumekuwa na changamoto mbalimbali zinazoikabili sekta ya elimu na hivyo kufanya hamasa katika utendaji wa walimu ishuke na vivyo hivyo kwa wanafunzi.
Ili kukabiliana na changamoto hizo, Serikali kupitia Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa pamoja ikishirikiana na Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu (Equip-Tanzania) imewekeza katika maendeleo ya sekta hiyo.Huu ni mpango unaotekelezwa na Serikali ili kuboresha mazingira ya mwanafunzi katika kujifunza ambao kwa sasa upo katika mikoa mitano ikiwemo Shinyanga, Tabora, Dodoma, Simiyu na Kigoma.
Itakumbukwa Equip-Tanzania ilianzishwa kwa malengo ya kutoa mafunzo na utendaji kazi kwa walimu pamoja na uongozi wa shule ambao tunashuhudia unavyoendelea kutekelezwa kupitia kwa walimu wakuu.
Pia inalenga kutekeleza mipango ya usimamizi wa elimu katika ngazi ya wilaya na mkoa kupitia kwa maofisa wake wa elimu ambao wanasimamia ngazi za chini yake zikiwemo kata.Mpango huo unalenga kuhakikisha kuwa ukusanyaji wa taarifa mbalimbali, takwimu na uwajibikaji katika suala zima la elmu mashuleni unafanyika ili kuboresha sekta hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Kishapu, Stephen Magoiga (kushoto) akiwa na wataalamu Afisa Mipango, Mang'era Mang'era na Afisa Elimu Msingi Wilaya, Sostenes Mbwilo wakipata maelezo kutoka kwa Afisa Elimu Ufundi, Moshi Balele kuhusu hatua za ujenzi wa chumba cha darasa shule ya msingi Migunga unajengwa pia kupitia nguvu za wananchi.
Mradi wa vyoo vya wanafunzi katika shule ya msingi ukikaguliwa na maafisa elimu kutoka Halmashauri ukiwa katika hatua za umaliziaji mbali ya kutumika kwa fedha za Serikali pia mradi huo umechangiwa na nguvu kazi ya wananchi.
Sehemu ya vyumba vya madarasa katika shule ya msingi Migunga ikiendelea kujegwa katika shule ya msingi Migunga ikiwa ni muendelezo wa mradi wa kuboresha huduma za sekta ya elimu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi
yaani makala yote Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/halmashauri-kishapu-yaboresha-huduma-za.html
0 Response to "Halmashauri Kishapu yaboresha huduma za elimu kupitia ushirikishaji wananchi"
Post a Comment