Loading...
title : ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO
link : ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO
ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
HALMASHAURI ya Manispaa ya Ilala Dar es Salaam imesema imetumia zaidi ya Sh.bilioni 5.5 kwenye utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa bajeti ya kuanzia Julai mwaka 2017 hadi Desemba mwaka huo.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu amesema fedha hizo zimetumika katika utekelezaji wa miradi inayohusisha ujenzi wa vyumba vya madarasa ,vyoo na hosteli.
"Kwa upande ya elimu ya msingi shule mpya nne zimejengwa kutokana na ongezeko la wanafunzi na ongezeko la wanafunzi ambalo limetokana na mpango wa Serikali wa elimu bila malipo,"amesema.
Pia ametaja kuwa katia mpango huo madarasa 28 yamejengwa katika shule za msingi Bonyokwa, Mongo la ndege, Mbondole, Mji Mpya, Kibaga, Bangulo na Misitu. "Madarasa sita yamefanyiwa ukarabati darasa moja Kinyerezi na Mchikichini vyumba vitano" amesema Tabu.
Amesema katika fedha hizo jumla ya matundu ya vyoo 96 yamejengwa katika shule hizo huku matundu 40 yakiwa katika shule za zamani na yaliyobakia katika shule mpya.
Shaibu ameongeza pia fedha hizo zimetumika kujenga mabweni kwa ajili ya wanafunzi wanaotoka mbali ili kukabiliana na changamoto ya usafiri wa wanafunzi wanaokaa maeneo ya mbali na shule.
Aamesema halmashauri imefanya ukarabati wa huduma za mama na mtoto katika zahanati ya Msongola na Mvuti kwa kutumia mapato ya ndani ikiwa pamoja na ukamilishaji na ukarabati wa miradi ya maji katika kata ya Minazi, Tabata, Majohe, Vingunguti, sekondari Pugu, Mkera na Pugu stesheni.
Amesema katika kipindi hicho halmashauri imepeleka kiasi cha Sh. 543,400,000 kwa ajili ya mikopo ya wanawake, vijana na walemavu na kukarabati miundombinu ya jijini Dar es Salaam kupitia mradi wa DMDP.
Afisa Uhusiano wa Manispaa ya Ilala, Tabu Shaibu, akizungumza juu ya taarifa ya utekelezwaji wa bajeti ya Halmashauri hiyo katika kipindi cha julai hadi Desemba 2017.
Waandishi wa Habari kutoka vyombo mbalimbali wakisikiliza kwa makini Taarifa hiyo ambayo inatolewa na Tabu Shaibu.
Hivyo makala ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO
yaani makala yote ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/ilala-yatumia-bilioni-55-utekelezaji-wa.html
0 Response to "ILALA YATUMIA BILIONI 5.5/- UTEKELEZAJI WA MAENDELEO"
Post a Comment