Loading...

JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA

Loading...
JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA
link : JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA

soma pia


JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA

MWAMBA WA HABARI
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.

Jaji kiongozi wa Mahakama ya Tanzania,Ferdinand Wambali amemtaka kila anayeomba kufanya kazi ya udalali wa mahakama kuwa na cheti cha umadhubuti katika kazi hiyo toka chuo cha uongozi wa Mahakama au taasisi inayotambuliwa na kamati ya uteuzi.
Jaji kiongozi, Ferdinand Wambali.

Amesema hayo leo wakati akifungua kongamano la wadau mbalimbali wa mahakama wanaoratibu na kusimamia utekelezaji wa amri za mahakama wakiwamo madalali.

Kongamano hilo limeratibiwa na Chuo cha uongozi wa Mahakama Lushoto kwa kushirikiana na Mahakama ya Tanzania lengo ni kujadili rasimu ya mtaala maalum wa kutolewa mafunzo kwa watu wanaofanya shughuli za udalali na usambazaji wito na amri za mahakama.

Jaji Wambali alisema mahakama inatambua madalali wa mahakama na wale wanaopaswa kupelekwa hati za kuitwa kwenye Mashauri wanawajibu kuhakikisha amri mbalimbali zinazotolewa na mahakama hasa katika Mashauri ya madai zinatekelezwa kwa mujibu wa sheria na kanuni zilizowekwa.

Alisema kuwa 1997 zilitungwa kanuni kuhusu uteuzi, maslahi na usimamizi wa madalali  wa mahakama na kwamba madalali wengi wanatekeleza majukumu yao bila ya kuwa na mafunzo rasmi ya kuwafanya wapate ujuzi wa utekelezaji wa kazi zao ukiacha ukiacha yale ya dharura yaliyofanyika 2003.

Alisema kuwa hiyo ilisababisha malalamiko kwa wadaawa na umma kuhusu mapungufu yaliyojitokeza ikiwamo ukiukwaji wa utaratibu na ukosefu wa maadili katika utekelezaji wa majukumu ya madalali.

Alibainisha kuwa hakuna shaka kuwa madalali wale waliopata kazi na kufanya usahili mbele ya kamati ya uteuzi, maslahi na usinamizi wa nidhamu ya maadili kwa ajili ya kutathmini sifa,uelewa na uwezo wao katika kutekeleza majukumu yao bado wengi hawakuwa na uelewa wa kutosha  kuhusu sheria na kanuni.

Alieleza kuwa kutokana na changamoto ambazo zilikabili wadau wa mahakama ilionekana upon umuhimu wa kufanya marekebisho ya namna ya kuwapata madalali, kusimamia nidhamu na maadili, maslahi na jinsi ya kutekeleza majukumu yao.

" Ni kwa sababu hiyo sheria ndogo namba 363 ya 2017 ilitungwa na kuchapishwa septemba 22,2017 na kuwa sheria hii ilifuta sheria ya 1997, ni matumaini yangu sheria hii itakuwa mwarobaini wa changamoto nyingi. " Alisema Jaji Kiongozi.

Pia alisisitiza kusema kuwa mtu anayeomba kufanya kazi ya udalali wa mahakama kuwa na cheti cha umadhubuti katika kazi hiyo toka chuo cha uongozi wa mahakama au taasisi nyingine yoyote inayotambuliwa na kamati ya uteuzi.

Jaji Kiongozi alitoa wito kwa washiriki katika mafunzo hayo ya siku mbili yanayofanyika Februari 16 na 17,2018 kushiriki kikamilifu na kwa dhati kwa kutoka maoni ya kuboreaha mtaala huo uliondaliwa bila kujali ngazi zao.

Alipendekeza mambo 15 kuwamo ndani ya mtaala huo ikiwamo utaratibu muhimu za uendeshaji wa Mashauri ya madai, aina za amri za mahakama zinazoweza kutolewa na matumizi ya teknolojia ya habari na Mawasiliano (Tehama).

Pamoja mahusiano kati ya madalali na maofisa wa mahakama na vyombo vingine vya dola, maadili ya kimahakama na mapambano dhidi ya rushwa pamoja na gharama zinazopaswa kutozwa kwa huduma za mahakama na watakazotoa madalali.

Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama  Dk Paul Kihwelo  alisema wao kama Chuo wanatumaini madalali na wasambazaji wito na amri za mahakama wataweza kuboresha utendaji wao wa kazi kupitia mafunzo hayo.

Alisema madalali wengi walitumia vibaya wigo wao kwa kutekeleza majukumu yao kinyume na matakwa ya kanuni kama vile kukamata mali zaidi ya zilizotajwa katika amri za mahakama, kuendesha minada kinyume cha utaratibu.


Hivyo makala JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA

yaani makala yote JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/jaji-kiongozi-awaonya-madalali-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JAJI KIONGOZI AWAONYA MADALALI WA MAHAKAMA"

Post a Comment

Loading...