Loading...
title : KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE
link : KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE
KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KAMATI ya Mashindano ya TFF imewafungia Deus Kaseke na Shaban Dihile kwa makosa ya utovu wa nidhamu waliyoyafanya katika mchezo wao wa Kombe la Shirikisho la Azam (FA).
Tukio hilo walilifanya wote kwa pamoja wakati wa mchezo wao kati ya Green Warriors na Singida United uliofanyika kwenye dimba la Azam Complex Chamazi jijini Dar es Salaam.
Kikao cha Kamati ya mashindano kilichokutana Februari 13 mwaka huu pamoja na mambo mengine iliweza kupitia taarifa za mchezo wa Kombe la Shirikisho la Azam kati ya Green Warriors na Singida United ambapo wachezaji Deus Kaseke wa Singida United na Shaban Dihile wa Green Warriors wamefungiwa mechi tatu (3) na faini ya Sh.500,000 kila mmoja kwa kosa la kutoingia uwanjani na timu zao na hawakuwepo wakati timu hizo zikipeana mikono kwenye mchezo uliozikutanisha timu hizo Januari 31,mwaka 2018 mchezo namba 73 uliochezwa Azam Complex Chamazi.
Adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni ya ASFC(1) ambayo inaelekeza kutumika kanuni ya ligi husika na hivyo kanuni iliyotumika ni 37(7d).
Mbali na hilo, mchezaji wa Singida United Kambale Salita amepelekwa kwenye Kamati ya nidhamu ya TFF kwa kosa la kumpiga mchezaji wa timu pinzani kwenye mchezo huo
Hivyo makala KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE
yaani makala yote KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/kamati-ya-mashindano-yawaadhibu-kaseke.html
0 Response to "KAMATI YA MASHINDANO YAWAADHIBU KASEKE, DIHILE"
Post a Comment