Loading...
title : KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU
link : KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU
KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
Shahidi wa pili wa Upande wa Mashtaka katika kesi ya kutumia dawa za kulevya inayomkabili msanii Wema Sepetu ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa aliijaza fomu ya kupima sampuli ya mkojo wa Wema, kabla hajamfanyia vipimo.
Aidha Shahidi huyo, Inspekta Wille, alidai kuwa hajawahi kupeleka sampuli za mkojo za washtakiwa Angelina Msigwa na Matrida Seleman Abbas ambao ni wafanyakazi wa Wema kwenda kuchunguzwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali kuhusu kukutwa na dawa za kulevya aina ya bangi.
Shahidi ameeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba alipokuwa akihojiwa na Wakili wa upande wa utetezi, Albert Msando baada ya kumaliza kutoa ushahidi wake.
Alipoulizwa muda gani alipeleka sampuli hiyo kwa Mkemia, alidai kuwa aliijaza fomu ya kupeleka sampuli ya mkojo wa Wema saa nne kamili asubuhi akiwa ofini kwao na kuandika maneno kuwa sampuli hiyo ya mkojo iko kwenye chupa ya plastiki lakini alikuwa bado hajampima mshtakiwa.
Alipoulizwa kama alijaza fomu hiyo kwa kuhisi tu, alidai, alijaza hivyo kwa kutumia uzoefu wake wa miaka 15 katika jeshi la polisi kwani alikuwa anajua taratibu za upimqaji ukifika katika ofisi ya Mkemia mkuu wa Serikali mkojo unakuwa katika chupa ya plastiki.

Aliendelea kudai kuwa Februari 8, mwaka jana alifika katika ofisi za Mkemia Mkuu wa Serikali saa tano asubuhi na kumkabidhi Mchunguzi Elia Mulima kichupa cha plastiki ambacho ndani kilikuwa na mkojo.
Wakili Msando alimuuliza shahidi ulikuwapo wakati sampuli ya mkojo uliokuwamo ndani ya kichupa cha plastiki unaodaiwa kuwa ni wa Wema ulipochukuliwa ambapo Inspekta Wille alidai kuwa hakuwapo.
Wakili Msando alimuuliza Inspekta Wille anaweza kusema kuwa unajua kwa uhakika kilichokuwa ndani ya chupa ya plastiki kuwa ni mkojo na je ni mkojo wa Wema? Alijibu kuwa hajui.
Msando alimuhoji Inspekta Wills kuwa walikaa kwa muda gani katika Ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Inpekta Wille alidai kuwa hakumbuki.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU
yaani makala yote KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/kesi-ya-wema-sepetu-kuunguruma-februari.html
0 Response to "KESI YA WEMA SEPETU KUUNGURUMA FEBRUARI 26 MWAKA HUU"
Post a Comment