Loading...
title : MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
link : MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeipiga kalenda kesi ya Uhujumu Uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.Bilioni 2.4, inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini nchini, Archard Kalugendo na mwenzake hadi Februari 27, mwaka huu.
Hatua hiyo, imekuja leo baada ya upande wa mashataka uliokuwa ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Estazia Wilson kuieieleza Mahakama kuwa jadala la kesi hiyo lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP)
Karugendo na mwenzeke, Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu wanakabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh.bilioni 2.4.
Baada ya kueleza hayo, Hakimu Godfrey Mwambapa aliahirisha kesi hiyo hadi Februari 27, mwaka huu itakapotajwa tena.
Inadaiwa kati ya Agosti 25 na 31, mwaka 2017 katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini wa madini waliisababishia hasara Serikali kiasi hicho cha fedha.
Hivyo makala MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI
yaani makala yote MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mahakama-yaipiga-kalenda-kesi-ya.html
0 Response to "MAHAKAMA YAIPIGA KALENDA KESI YA UHUJUMU UCHUMI"
Post a Comment