Loading...
title : PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA
link : PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA
PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA
Na Anitha Jonas – WHUSM.
Serikali yatao Milioni Mia saba kwa ajili ya ukarabati wa Jengo lilokuwa Makao Makuu ya Wanakamati wanaopigania Uhuru wa kulikomboa Bara la Afrika ikiwa ni sehemu ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika.
Kauli hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt.Harrison Mwakyembe alipotembelea ofisi zinazoratibu programu hiyo ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika leo jijini Dar es Salaam kupata taarifa ya maendeleo ya programu hiyo.
‘’Tumepewa dhamana na heshima kubwa na Umoja wa Afrika ya kuhifadhi historia ya Ukombozi wa Bara la Afrika sababu ya Baba wa Taifa Hayati Julius Nyerere alivyopigania uhuru wa bara la afrika na kutoa ofisi jijini Dar es Salaam ambayo ilikuwa Makao Makuu ya wapigania Uhuru kutoka nchi mbalimbali za Afrika kukutania na kupanga mikakati hivyo ni vyema tuhifadhi historia hii,’’ Dkt.Mwakyembe.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akizungumza na waandishi wa Habari (hawapo pichani) kuhusu Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika ambao utakuwa ukikusanya na kuhifadhi historia ya ukombozi wa bara la Afrika alipotembelea yaliyokuwa Makao Makuu ya Ofisi za Wanakamati wa Ukombozi wa Bara la Afrika zilizopo jijini Dar es Salaam leo,kushoto kwake ni Naibu Katibu Mkuu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bw. Nicholaus Wiliam.
Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe akiwaeleza waandishi (hawapo pichani) kuhusu historia ya pikipiki aliyoshika kuwa ilikuwa ikitumiwa na Rais wa awamu ya kwanza wa Msumbiji Hayati Samora Machel katika kipindi cha kupigania uhuru wanchi yake, alipotembelea yaliyokuwa Makao Makuu ya Ofisi za Wanakamati wa kukomboa Bara la Afrika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Idara ya Historia na Makumbusho (JWTZ) Kanali Robert Mjange (wa pili kulia) akimweleza Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia) kuhusu hali ya jengo ambalo lilikuwa ni Makao Makuu yaliyokuwa yakitumiwa na viongozi mbalimbali wa Afrika ambao walikuwa wanakamati wa kupigania Ukombozi wa Bara la Afrika hapo zamani, alipotembelea Ofisi zinazoratibu Programu ya Ukombozi Bara la Afrika zilizopo jijini Dar es Salaam kupata taarifa ya maendeleo ya programu hiyo.
Mratibu wa Programu ya Urithi na Ukombozi wa Bara la Afrika Bibi Ingiahedi Mduma (katikati) akimwonyesha Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe (kulia) jengo ambalo lilikuwa ni Makao makuu ya Viongozi wa Kamati ya kupigania uhuru wa bara la afrika hapo zamani ambalo linahitaji ukarabati kwa sasa alipotembelea ofisi zinazoratibu programu hiyo leo jijini Dar es Salaam.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA
yaani makala yote PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/programu-ya-urithi-wa-ukombozi-wa-bara.html
0 Response to "PROGRAMU YA URITHI WA UKOMBOZI WA BARA LA AFRIKA KUIJENGEA HESHIMA TAIFA"
Post a Comment