Loading...
title : MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI
link : MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI
MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI
Na Said Mwishehe, Glogu ya jamii
WABUNGE kutoka majimbo mbalimbali nchini kupitia Chama ChaMapinduzi (CCM), wamewaomba wananchi wa jimbo la Kinondoni jijiniDar es Salaam kuhakikisha Februari 17, mwaka huu wanamchaguamgombea ubunge wa chama hicho, Abdallah Mtulia katika uchaguzi
mdogo jimboni humo.
Wamesema Mtulia ndio chaguo sahihi kwa wananchi wa Kinondoni nakwamba akiwa mbunge watashirikiana naye katika kufanikishachangamoto za wananchi zinapata ufumbuzi wake.Pia wameeleza namna ambavyo wabunge wa CCM wamekuwa wamojabungeni katika kupigania maendeleo ya wananchi tofauti na wabungewa upinzani ambao kila kitu wao ni kupinga hata liwe jambo lamaendeleo.
Wakizungumza kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika wanja wa People Kigogo wilayani Kinondoni jijini, wabunge hao waCCM wamewaomba wananchi kutofanya makosa kwenye uchaguzi huohuku wakitoa sababu mbalimbali za kwanini Mtulia anastahili kuwa mbunge wa jimbo hilo.
Mgeni rasmi kwenye kampeni hizo ambaye pia ni Mbunge wa Nzega Mjini, Hussein Bashe (CCM) amewaomba wananchikumchagua Mtulia kwani ndio mgombea sahihi na wanaamini akiwambunge watashirikiana naye kutatua kero za wananchi.
"Nimekuja kuzungumza na ninyi kuwaomba tarehe 17,siku yaJumamosi wote mkamchague Mtulia, lakini si tu kumchagua lazimatuseme kwanini mumchague Mtulia.Ndio mgombea mwenye sifa zoteza kuwa mbunge wa Kinondoni,"amesema Bashe.
Pia amesema kwenye kampeni hizo wapo wanaotoa hoja kuwa Serikali ya CCM haitaki mfumo wa vyama vingi, ambapo amefafanua hoja hiyo haina maana yoyote kwani mwaka 1992 licha ya watanzania wengi kutaka mfumo wa chama kimoja uendelee lakini uamuzi ulitolewa wa kuingia mfumo vyama vingi.
"Mwaka 1992, watanzania walipata fursa ya kuchagua tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi au laa.Waliotaka vyama vingi walikuwa asilimia 20 na waliosema chama kimoja kiendelee walikuwa asilimia 80."Mwaka 1995 tukafanya uchaguzi wa vyama vingi na CCM ikashinda, hivyo CCM hatuna hofu na mfumo wa vyama vingi na ndio maana tumeendelea kushinda katika kila chaguzi.
"Pia wapo wanaotoa hoja CCM hakuna demokrasia hili nalo halina ukweli.CCM demokrasia ipo tena ya kutosha.Ndani ya CCM tunaweza kutofautiana kimtazamo, tunaweza kutofautiana kwa hoja na wakati mwingine tukashikana mashati lakini ukweli utabaki tunafanya hayo yote kwasababu ya demokrasia tuliyonayo,"amesema Bashe.
Hivyo makala MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI
yaani makala yote MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mama-salma-bashe-msukuma-lusinde.html
0 Response to "MAMA SALMA, BASHE, MSUKUMA, LUSINDE WAMUOMBEA KURA MTULIA KINONDONI"
Post a Comment