Loading...
title : MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO
link : MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO
MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO
Mgodi wa dhahabu wa Acacia Bulyanhulu umezindua na kukabidhi maktaba iliyogharimu shilingi milioni 22.6 kwenye shule ya sekondari Bulyanhulu iliyopo katika halmashauri ya Msalala wilayani Kahama mkoani wa Shinyanga kwa lengo la kusaidia wanafunzi na walimu katika kuboresha ubora wa elimu inayotolewa.
Maktaba hiyo imezinduliwa na Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Msalala Bw , Simon Berege na kuhudhuriwa na kaimu Meneja mkuu wa Mgodi wa Bulyanhulu,Elias Kasitila.
Akizungumza wakati uzinduzi huo, Kaimu Meneja Mkuu wa Mgodi Bulyanhulu,Elias Kasitila alisema wakati wakitafakari namna ya kuinua taaluma ya wanafunzi waliona ni vyema wakaimarisha usomaji wa wanafunzi kwa kuwekeza kwenye maktaba ambayo itasaidia kuboresha upatikanaji wa elimu kwa wanafunzi kutoka kwa jamii inayouzunguka mgodi huo.
Alisema kupitia mpango wa Acacia wa maendeleo ya jamii wameamua kushirikiana na shirika la kimataifa la Read International kuboresha jengo moja la shule hiyo na kuliwekea samani kwa ajili ya matumizi ya maktaba ambayo itawasaidia wanafunzi na walimu kwa kiasi kikubwa.
Mkurugenzi wa halmashauri ya Msalala ,Simon Berege akikata utepe kuzindua rasmi jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu. Kaulia ni kaimu Meneja mkuu wa mgodi wa Bulyanhulu Elias Kasitila.Na katikati ni Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi .
Muonekano wa jengo la maktaba katika shule ya sekondari Bulyanhulu lililoboreshwa na mgodi wa Bulyanhulu kwa kushirikiana na Read International .
Mwakilishi wa shirika la Read International ,Esther Kalwinzi akionesha sehemu ya kuangalia orodha ya aina za vitabu vilivyopo katika maktaba kwa mkurugenzi wa halmashauri ya msalala , Simon Berege .
Hivyo makala MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO
yaani makala yote MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mgodi-wa-acacia-bulyanhulu-waendelea.html
0 Response to "MGODI WA ACACIA BULYANHULU WAENDELEA KUSHIRIKIANA NA JAMII MIRADI YA MAENDELEO"
Post a Comment