Loading...
title : MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI
link : MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI
MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, ameitaka kampuni ya Huduma za Meli (MSCL) kuhakikisha inafunga kamera katika maeneo mbalimbali ya ukaguzi ili kudhibiti vitendo vya hujuma katika mifumo ya kampuni hiyo hususani kwenye Mapato.
Ametoa rai hiyo jijini Mwanza mara baada ya kuzindua mfumo mpya wa ukatishaji tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV Clarias na kusisitiza kuwa matumizi ya mfumo huo mpya yaende sambamba na elimu stahiki kwa watumishi wanaoutumia mfumo huo katika kukatisha tiketi.
“Niwapongeze sana kwa hatua hii ya kuingia kwenye mfumo wa kielektroniki katika utoaji huduma lakini niwatake sasa kuongeza kamera kwenye maeneo yote unapofanyika ukaguzi ili kudhibiti mianya yote inayoweza kujitokeza ya kuhujumu mapato ya kampuni” amesema Prof. Mbarawa.
Ameongeza kuwa Serikali itaendelea kuwekeza kwenye shirika hilo ili liweze kupata faida na liweze kujitegemea na kuagiza kuwa kwa sasa kila fedha inayopatikana itumike vizuri sababu Shirika limeanza kupata faida.
Aidha, Prof. Mbarawa amemtaka Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Serikali Mtandao (eGA), kutengeneza mfumo kama huo kwa ajili ya Shirika la Reli Nchini (TRL), ili kudhibiti uvujaji wa mapato.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa ukatishaji wa tiketi kwa njia ya kielektroniki katika Meli ya MV. Clarias inayotoa huduma kati ya Mwanza na Ukerewe.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akikata tiketi ya kieletroniki mara baada ya kuzindua mfumo wa tiketi hizo katika Meli ya MV Clarias, mkoani Mwanza.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo kwa Kaimu Meneja Mkuu wa kampuni ya Huduma za Meli (MSCL), Bw. Erick Hamis, wakati akikagua ukarabati wa Meli ya MV. Clarias, mkoani Mwanza.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI
yaani makala yote MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/mscl-kudhibiti-mapato-kielektroniki.html
0 Response to "MSCL KUDHIBITI MAPATO KIELEKTRONIKI"
Post a Comment