Loading...
title : NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO
link : NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO
NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO
Na Ripota Wetu, Arusha
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Arusha Charles Mkumbo amepata ajali ya gari katika eneo la Mdori mkoani Manyara.
Taarifa kuhusu tukio hilo zinadai kuwa Kamanda Mkumbo amepata ajali leo, baada ya gari aliyokuwa akiitumia kupasuka gurudumu la nyuma.
Baada ya kupasuka kwa gurudumu hilo, gari ilipoteza muelekeo na kisha kupinduka.Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Yusuph Ilembo amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo.
Ambapo amesema ndani ya gari hiyo kulikuwa na watu watatu akiwamo Msaidizi wa Kamanda Mkumbo pamoja na dereva wake na kwamba hali zao zinaendelea vizuri.
Ilembo amesema ajali hiyo imetokea leo saa nane mchana wakati Kamanda Mkumbuko akiwa njiani kutokea mkoani Singida kwenda Arusha na alipofika eneo la katikati ya Mdori na Minjingu ndipo guruduma la nyuma upande wa kushoto la gari hiyo lilipasuka na kusababisha ajali hiyo.
Amesema Kamanda Mkumbo ameumia kidole chake cha shahada na baada ya ajali hiyo amepelekwa Hospitali hiyo ya Mkoa wa Arusha ambako anaendelea na matibabu wakati dereva wake naye analalamika maumivu kwenye paja la upande wa kushoto na msaidizi wake anasema hajaumia kwani hasikii maumivu mahali popote.
Amewataka wananchi wa Arusha kutokuwa na hofu kwani Kamanda Mkumbo hali yake inaendelea vema na kubwa ni kumuombea ili arudi kwenye hali yake ya kawaida na kuendelea na majukumu mengine ya kulitumikia Taifa.
Baadhi ya Wananchi wakishuhudia tukio a ajali hiyo.
Hivyo makala NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO
yaani makala yote NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/newz-alertrpc-arusha-apata-ajali-baada.html
0 Response to "NEWZ ALERT:RPC ARUSHA APATA AJALI BAADA YA GARI YAKE KUPOTEZA MUELEKEO"
Post a Comment