Loading...

PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI

Loading...
PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI
link : PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI

soma pia


PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI

Na Mwandishi Wetu. IDARA ya uhamiaji nchini imewataka watanzania kupuuza habari zinazozagaa kuhusu uvumi wa pasipoti mpya kuwa zimechakachuliwa.

Kauli hiyo ameitoa leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala amesema wananchi wanatakiwa kupata taarifa sahihi kila mara juu ya kila jambo linalohusu maendeleo yao na mambo yanayoletea ustawi wa Taifa letu,sisi ndio wenye taarifa sahihi zinazohusu Mchakato mzima wa Pasipoti Mpya za Kielektroniki

Hivi karibuni Rais Dkt. John Magufuli wakati akizindua hati mpya za kusafiria alisema kumekuwapo na wahujumu wa mchakato huo ambao hawakufanikiwa kuiba sh. bilioni 400.Amesema kumekuwapo kwa watu waliozunguka kila kona na kutumia kila njama zote kupiga vita mchakato huo wakidhani watafanikiwa kuhujumu serikali.

Dkt. Anna Makakala amesema hatua hizo za kutoa na kueneza taarifa zisizo sahihi zinawaletea mkanganyiko wananchi na kudhoofisha mawazo na fikra chanya kwa Taifa lao.Amesema ni vyema jamii kutambua kuwa mchakato wa Pasipoti mpya ya kidigitali ni hatua kubwa kwa Taifa hili na si vyema kuutolea Taarifa zisizo sahihi, amewasihi wanahabari kupata taarifa kutoka katika vyanzo sahihi na kuzifikisha kwa walaji ambao ni Wananchi," 

Amesisitiza hatua ya mafanikio ya matumizi ya hati hizo hazitarudi nyuma kwa sababu ya kuwapo na taarifa zisizo sahihi zenye lengo la kupotosha ukweli wa mchakato huo.“Ni vyema jamii kuelewa kazi ya hati hizo ni kulinda usalama wa nchi yetu hivyo Uhamiaji tutaendelea kudhibiti mipaka ya Tanzania na kulinda usalama wa nchi kwa kuwezesha jamii na raia wa kigeni kufuata taratibu katika utokaji,ukaaji na uingiaji wa kila mmoja,” amesema Dkt. Makakala.

Kamishna Jenerali wa Uhamiaji nchini, Dkt. Anna Makakala akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam.



Hivyo makala PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI

yaani makala yote PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/pasipoti-mpya-ni-salama-asilimia-100.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "PASIPOTI MPYA NI SALAMA ASILIMIA 100: UHAMIAJI"

Post a Comment

Loading...