Loading...
title : Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi
link : Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi
Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi
Timu ya Zesco United kutoka Zambia katika picha
Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.
Wapinzani wa JKU katika michuano ya Klabu Bingwa Afrika timu ya Zesco United kutoka Zambia wamewasili leo Zanzibar tayari kabisa kwa mchezo wa Jumamosi kwenye uwanja wa Amaan.
Timu hiyo imewasili leo saa nne asubuhi kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume kwa ndege ya Shirika la Ndege la Kenya ambapo wachezaji wa timu hiyo wameongozana na viongozi wao na wamepokelewa na wenyeji wao ambao ni viongozi wa timu ya JKU.
Afisa habari wa chama cha soka Zanzibar (ZFA) Ali Bakar (Cheupe) amesema kwa upande wao Chama maandalizi yote wamekamilisha huku akiwataka Mashabiki wa soka kujitokeza kwa wingi kwenda kuzishangiria timu za Zanzibar.
Wawakilishi wa Zanzibar katika Mashindano hayo ya Kimataifa ni JKU ambao wataivaa Zesco United siku ya Jumamosi katika mchezo wa kombe la Klabu bingwa huku Zimamoto ambao watawakilisha kwenye kombe la Shirikisho wataivaa Walaitta Dicha ya Ethiopia siku ya Jumapili michezo yote itapigwa majira ya saa 10:00 za jioni katika uwanja wa Amaan.
Hivyo makala Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi
yaani makala yote Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/zesco-united-yawasili-zanzibar-tayari.html
0 Response to "Zesco United yawasili Zanzibar tayari kuwavaa JKU Jumamosi"
Post a Comment