Loading...
title : SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA
link : SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA
SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Dkt. Laurean Ndumbaro amewaelekeza Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kufanya mapitio na ukaguzi wa zoezi la uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma katika Halmashauri zao.
Lengo la maelekezo hayo ni kujiridhisha na sifa za watumishi waliojiriwa kwa cheti cha darasa la saba na walioajiriwa kwa sifa ya cheti cha ufaulu wa Kidato cha Nne kama wamewasilisha vyeti vyao na kuhakikiwa.Dkt. Ndumbaro ametoa maelekezo hayo katika kikao kazi na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe.
Dkt. Ndumbaro ametoa angalizo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa nchini kuhakikisha wanawaondoa katika Utumishi wa Umma watumishi ambao hawajawasilisha vyeti vya Kidato cha Nne kwa ajili ya uhakiki na wale waliodanganya kuwa ni darasa la saba ili kukwepa zoezi la uhakiki wa vyeti vya kidato cha Nne,Sita na Ualimu.
Dkt. Ndumbaro amesisitiza kuwa, ofisi yake itatoa Waraka wa kuzitaka Mamlaka za Sekretarieti za Mikoa kwenda kufanya ukaguzi katika Halmashauri zao ili kujiridhisha na namna zoezi la uhakiki liliyofanyika.
Katibu Mkuu Dkt. Ndumbaro katika kikao kazi hicho amepokea changamoto mbalimbali na kuzitolea ufafanuzi ili kuleta mabadiliko ya utendaji kazi katika Utumishi wa Umma nchini.
Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaroakizungumza na watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe katika kikao kazi na waumishi hao chenye lengo la kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
Baadhi ya watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe wakimsikiliza Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) katika kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kuwasikiliza na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
Mmoja wa watumishi wa Sekretarieti ya Mkoa wa Njombe akiwasilisha hoja yake kwa Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma Dkt. Laurean Ndumbaro (hayupo pichani) wakati wa kikao kazi na watumishi hao chenye lengo kusikiliza changamoto zinazowakabili watumishi hao na kutoa ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi.
Imetolewa na James Katubuka Mwanamyoto
Afisa Habari
Ofisi ya Rais-UTUMISHI na Utawala Bora
Hivyo makala SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA
yaani makala yote SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/serikali-yaelekeza-makatibu-tawala-wa.html
0 Response to "SERIKALI YAELEKEZA MAKATIBU TAWALA WA MIKOA KUFANYA UKAGUZI WA ZOEZI LA UHAKIKI WA VYETI VYA WATUMISHI WA UMMA"
Post a Comment