Loading...
title : SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA
link : SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA
SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA
Na Lydia Churi-Mahakama, Kigoma
Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma ameishauri Serikali kuishirikisha Mahakama ya Tanzania kwenye mipango yake ya uanzishaji wa maeneo mapya ya kiutawala ili kupunguza changamoto za upatikanaji wa haki kwa wananchi.
Akizungumza wakati wa ziara yake mjini Kigoma, Jaji Mkuu amesema mipango ya Serikali ya uanzishwaji wa wilaya au mikoa izingatie pia uanzishwaji wa Mahakama. Aliongeza kuwa Mikoa na wilaya mpya ndizo zenye ukosefu wa Mahakama hali inayowafanya wananchi kufuata mbali huduma za kimahakama.
Alisema Mahakama kupitia Mpango Mkakati wake wa miaka mitano (2015/16 hadi 2019/20) imejipanga kutatua tatizo la ukosefu wa huduma za Mahakama pamoja na kusogeza huduma hizo karibu Zaidi na wananchi. Kwa kushirikiana na Benki ya Dunia, tayari imeanza ujenzi wa Mahakama tano za Hakimu Mkazi katika mikoa ya Simiyu, Katavi, Geita, Njombe na Manyara pamoja na ujenzi wa Mahakama 16 za wilaya na Mahakama Kuu mbili katika Mikoa ya Kigoma na Mara.
Jaji Prof. Juma amesema kupitia ziara yake ya siku saba kwenye Mahakama Kuu kanda ya Tabora amebaini kuwa watanzania wengi hufuata mbali huduma za Mahakama na maeneo mengine ni kutokana na jiografia ya maeneo hayo. Akitolea mfano wa wilaya ya Uyui mkoani Tabora, Jaji Mkuu amesema kutokana na wilaya hiyo kuzunguka mkoa, wananchi wake hulazimika kufuata huduma za Mahakama Kuu zilizopo umbali wa Zaidi ya kilometa 377.
Jaji mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwa pamoja na wakandarasi wa kampuni ya Masasi Contruction Ltd wanaojenga jengo la mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Kigoma. mahakama ya Tanzania inajenga jengo hili pamoja na mengine nchini ili kusogeza huduma za mahakama karibu zaidi na wananchi.
Hivyo makala SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA
yaani makala yote SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/serikali-yashauriwa-kuishirikisha.html
0 Response to "SERIKALI YASHAURIWA KUISHIRIKISHA MAHAKAMA KWENYE UANZISHWAJI WA MIKOA NA WILAYA"
Post a Comment