Loading...
title : Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe.
link : Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe.
Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe.
Na Agness Francis Globu ya jamii
VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba Sc wanaendelea kujifua vikali kukabiliana na mchezo wao kimataifa dhidi ya Gendarmerie Nationale FC ya nchini Djibouti katika kuwania Kombe la Shirikisho la CAF.
Mtanange huo utakaorindima Februari 11 katika Dimba la Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam Majira ya Saa 10:00 jioni .
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam katika Makao Makuu ya Timu ya SimbaSc' Mnyama' Msemaji Mkuu wa Timu ya Simba, Hajji Manara amesema kuwa katika mchezo huo atahudhuriwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Dk. Ali Hassan Mwinyi akiwa kama Mgeni rasmi katika mchezo huo.
"Timu yetu ipo vizuri na kikosi kipo kinaendelea na mazoezi na vijana wapo fiti kabisa ukizingatia wachezaji wetu tayari wawili Saidi Nduda pamoja na Salimu Mbonde wanaendelea vizuri na wamesharejea kikosini kuendelea na na Mazoezi"amesema Manara.
Hata hivyo katika mtanange huo wataendelea kumkosa nyota wao kutoka Rwanda Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni ataelekea Nchini India kwa ajili ya matibabu .
"Tutaendelea kumkosa Mchezaji wetu mahiri Haruna Niyonzima ambaye hivi karibuni ataelekea Nchini India kwa ajili ya matibabu ya maradhi yanayomsumbua, ila mpaka kufikia mwezi ujao atarejea kikosini"amesema Manara.
Aidha Manara amesema kuwa Timu ya Gendarmerie Nationale FC watawasili Jumamosi saa 7:00 Usiku ambapo msafara wao utakuwa ni wa watu 18 na Viongozi wakiwa ni 8.
Katika Mtanange huo Manara amewasaa mashabiki kuhudhuria kwa wingi katika mchezo huo ambapo viingilio vitakuwa ni Sh,30,000 kwa VIP A, Sh.20,000 kwa VIP B, Viti vya rangi ya Chungwa 'Orange' Sh.10,000 na Sh.50,00 kwa vitu vya Mzunguko.
Hivyo makala Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe.
yaani makala yote Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/simba-sc-gendarmerie-nationale-nani.html
0 Response to "Simba Sc, Gendarmerie Nationale Nani Mbabe."
Post a Comment