Loading...
title : Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani
link : Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani
Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga ametoa wito kwa Jumuiya ya Kimataifa kuisaidia Tanzania kutokana na mchango mkubwa wa kuwahudumia wakimbizi ambao imekuwa ikiutoa kabla na baada ya uhuru, licha ya uchumi mdogo ilio nao.
Waziri Mahiga ametoa wito huo leo Jijini Dar Es Salaam katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani (World Refugees Council-WRF) kinachofanyika kwa siku mbili kuanzia jana kwenye Hoteli ya Hyatt Regecy, Kilimanjaro.
Waziri Mahiga alieleza kuwa Tanzania ilipokea wakimbizi kutoka Poland wakati wa vita ya pili ya dunia na mwaka 1959 ilipokea wakimbizi kutoka nchi ya Rwanda. Aidha, baada ya uhuru, Tanzania imekuwa ikipokea wakimbizi mara kwa mara na wakati wa mauaji ya kimbari nchini Rwanda, Tanzania ilipokea wakimbizi wengi zaidi duniani.
Aliendelea kueleza kuwa athari zinazotokana na kupokea wakimbizi wengi ni nyingi na kubwa hivyo, ni jukumu la Jumuiya ya Kimataifa kuzisaidia nchi zenye wakimbizi wengi, hususan zile zenya uchumi mdogo.
Rais Mstaafu wa awamu ya nne, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete akiongea katika kikao cha Baraza la Wakimbizi Duniani kinachofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency, Kilimanjaro jijini DAr es salaam.
Kwa habari kamili BOFYA HAPA |
Hivyo makala Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani
yaani makala yote Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/tanzania-yawa-mwenyeji-ya-mkutano-wa.html
0 Response to "Tanzania yawa Mwenyeji ya Mkutano wa Baraza la Wakimbizi Duniani"
Post a Comment