Loading...

UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

Loading...
UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI
link : UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

soma pia


UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

Na Veronica Simba – Dodoma
Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Nishati na Kampuni ya Total wamekubaliana kuharakisha hatua zote za awali katika Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima Tanga ili shughuli za ujenzi rasmi zianze mwezi Mei mwaka huu.
Makubaliano hayo yalifikiwa Alhamisi, Februari 1, wakati Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani alipokutana na uongozi wa juu wa kampuni hiyo wizarani Dodoma.
Aidha, makubaliano mengine yaliyofikiwa katika kikao hicho ni kuwa kazi za awali za maandalizi ya ujenzi ziwe zimekamilika ifikapo mwezi Machi mwaka huu.
“Ni lazima tuharakishe mchakato huu kama Mheshimiwa Rais Magufuli alivyoagiza. Hivyo, tumekubaliana kwamba shughuli zote za maandalizi ziwe zimekamilika ifikapo Machi mwaka huu ili kuwezesha shughuli rasmi za ujenzi wa Bomba kuanza mwezi Mei,” alifafanua Waziri Kalemani.
Vilevile, katika kikao hicho, Rais wa Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy Maurice ambaye alikuwa kiongozi wa Ujumbe huo, alibainisha nia ya kampuni yake kuwekeza katika shughuli nyingine mbalimbali zinazohusiana na Mradi wa Bomba jambo ambalo alisema litainufaisha zaidi Tanzania.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (katikati), akiongoza kikao baina ya viongozi na wataalam wa Wizara (kulia) na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total (kushoto). Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.
 Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto), akimsikiliza Rais wa Kampuni ya Total sehemu ya Afrika, Guy Maurice (kulia) wakati wa kikao baina yao kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu.
 Viongozi na wataalam wa Wizara ya Nishati, wakiwa katika kikao baina ya Wizara na Ujumbe kutoka Kampuni ya Total kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).
Ujumbe kutoka Kampuni ya Total wakiwa katika kikao baina yao na Viongozi na wataalam wa Wizara ya Nishati kujadili utekelezaji wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Hoima-Tanga. Kikao hicho kilifanyika Makao Makuu ya Wizara mjini Dodoma, Februari Mosi, mwaka huu na kiliongozwa na Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (hayupo pichani).



Hivyo makala UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI

yaani makala yote UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/ujenzi-rasmi-bomba-la-mafuta-kuanza-mei.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "UJENZI RASMI BOMBA LA MAFUTA KUANZA MEI"

Post a Comment

Loading...