Loading...
title : Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC
link : Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC
Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo amesema maboresho ya TEHAMA yanayofanywa na mhimili wa mahakama nchini utasaidia kupunguza foleni za wananchi wanaofika ofisi za Wakuu wa Wilaya na kwa Mkuu wa Mkoa kutafuta haki zao.
Amesema kuwa kitendo cha mwaanchi kuweza kujua mwenendo wa kesi bila ya kufika mahakamani ni maendeleo makubwa yanayofikiwa na mhimili huo na kuwaasa kuanza kufanya kazi baada ya kuwa likizo ya mwisho wa mwaka.
Ameyasema hayo kwenye maadhimisho ya wiki ya sheria ambayo hufanyika tarehe 1, Februari ya kila mwaka katika Viwanja wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi.
“Mwaka 2018 na jitihada zilizofanyika na mahakama umekuwa mwanzo mzuri, wananchi watajitokeza kutafuta elimu hii ya sheria na wanapoipata itatupunguzia msongamano kwenye ofisi zetu za Mkuu wa Wilaya na Mkuu wa Mkoa ili tufanye kazi za maendeleo sio kusuluhisha migogo ya ndoa, mirathi na ardhi ambayo yote imekaa katika misingi ya kisheria,” Alieleza.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akizungumza wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Sheria yaliyofanyika katika Viwanja wa mahakama kuu ya Tanzania kanda ya Sumbawanga inayojumuisha mikoa ya Rukwa na Katavi..
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo (wa tatu kutoka kulia) akiwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga John Mgeta (wa kwanza kushoto) na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga Dk. Adam Mambi (wa pili kutoka kulia) na Mwanasheria wa Serikali mkoa wa Rukwa Prosper Regerera.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mh. Joachim Wangabo akisalimiana na Jaji Mkuu wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Sumbawanga Dk. Adam Mambi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC
yaani makala yote Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/matumizi-ya-tehama-kusaidia-kupunguza.html
0 Response to "Matumizi ya TEHAMA kusaidia kupunguza msongamano ofisi za DC na RC"
Post a Comment