Loading...
title : UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA
link : UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA
UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA
BENKI Kuu ya Tanzania(BoT) imesema bado ni changamoto kwa watanzania walio wengi katika kutunza fedha za noti na noti ya sh.500 na noti ya Sh.1000.
Hayo yamesemwa leo mkoani Mtwara na Meneja Msaidizi Idara ya Sarafu kutoka Benki Kuu Tanzania(BoT) Dolla Abdull wakati akitoa mada kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye semina iliyoandaliwa na benki hiyo kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kuandika taarifa sahihi za uchumi.
Akifafanua kuhusu fedha chakavu, amesema noti ya Sh.500 ndio inayochakaa zaidi ukilinganisha na noti nyingine inayofuata kwa kuchakaa ni ya Sh.1000.Amesema sababu ya fedha hizo kuchakaa haraka inatokana na kutumika zaidi kwenye mzunguko wa fedha hasa kwa kuzingatia kundi kubwa la wananchi ndio watumiaji wakubwa.

Amefafanua sababu nyingine ya fedha hizo kuchakaa haraka inatokana na ukweli uliopo watanzania ambao wwnatunza fedha zao benki hawazidi asilimia 14.Hivyo amesema sehemu kubwa ya fedha inabaki mtaani na matokeo yake zinachakaa. "Ujue fedha nayo ina umri wake wa kuishi ambapo kwa fedha za noti ni zinaishi kati ya miezi sita hadi saba.
" Kazi yetu idara ya sarafu ni kuhakikisha tunapeleka fedha safi katika mzunguko na zile ambazo zimechakaa tunazisaga katika mashine maalumu,"amesema Dolla.
Ametoa ombi kwa Watanzania kuhakikisha wanatunza fedha hizo kwani Serikali inatumia gharama kubwa kuchapa fedha hizo huku akifafanua fedha ni moja ya alama ya nchi yetu,hivyo lazima zitunzwe vizuri.Amesititiza wananchi kutunza fedha zao benki kwani ni njia moja wapo ya kuzifanya fedha kuwa safi huku akiwakumbusha wenye fedha zilizochaa kuzipeleka benki ili zibadilishwe.
Hivyo makala UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA
yaani makala yote UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/utunzaji-fedha-bado-ni-changamoto-kwa.html
0 Response to "UTUNZAJI FEDHA BADO NI CHANGAMOTO KWA WATANZANIA"
Post a Comment