Loading...
title : WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA
link : WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA
WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA
Mkuu wa Wilaya ya Kondoa Mh. Sezaria Makota amesema hatowafumbia macho wale wote wenye nia ya kuishusha wilaya ya Kondoa kielimu kwa kuvuruga kwa makusudi mikakati ya kuinua elimu wilayani humu.
Aliyasema hayo wakati wa kikao cha wadau wa elimu wa Halmashauri ya Mji Kondoa kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa elimu ili kujadili changamoto na mikakati ya kuinua elimu ndani ya Wilaya ya Kondoa.
Alisema kuwa katika utawala wake hatoruhusu elimu kushuka kwani matokeo ya darasa la saba mwaka jana wilaya imeshuka kiwastani ukilinganisha na mwaka juzi ambapo wilaya ilikuwa na wastani wa asilimia 80 na mwaka jana imeshuka na kufikia asilimia 71 hivyo viongozi wajipange kusimamia elimu ili kuhakikisha ufaulu unapanda.
Aidha aliwaagiza maafisa elimu kumpelekea mipango yao ili kuona jinsi gani wanainua elimu na kutaka viongozi wa Halmashauri kuacha migogoro na kutekeleza mipango kwa vitendo ili kufikia mafanikio katika elimu.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kwapakacha Mwalimu Pantaleo akisoma barua katika kikao cha wadau wa elimu iliyoandikwa na mwanafunzi wa kidato cha pili akielezea sababu za kutaka kuacha shule.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji Kondoa akimwelekeza Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Tungufu kupandisha ufaulu baada ya kupokea cheti cha shule yenye ufaulu duni Wilayani katika kikao cha wadau wa elimu kilichofanyika katika ukumbi wa Kondoa Irangi hivi karibuni.
Katibu Tawala Wilaya ya Kondoa, Winnie Kijazi akimpa zawadi mmoja ya walimu waliofaulisha kwa alama A katika mtihani wa darasa la saba mwaka 2017 kwenye kikao cha wadau wa elimu.
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
HABARI ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA
yaani makala yote WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/wavuruga-elimu-kondoa-wamkera-mkuu-wa.html
0 Response to "WAVURUGA ELIMU KONDOA WAMKERA MKUU WA WILAYA"
Post a Comment