Loading...
title : WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
link : WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
SERIKALI ya Wilaya ya Kaliua imewaagiza Watendaji kuanzia kazi za vijiji hadi Kata kuhakikisha wanaendesha msako wa kuwakata wazazi wote ambao watoto wao watakuwa hawajaripoti shuleni hadi mwisho wa Mwezi wa Pili mwaka huu.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mkuu wa Wilaya Abel Busalama wakati akizungumza na Madiwani na Wakuu wa Idara wa Halmashauri ya Kaliua.
Alisema kuwa baada ya muda huo kuisha wanatakiwa kukamata watoto wote wenye umri wa kuwa shuleni ambao wanazurura mitaani au kutumikishwa katika shughuli za biashara.
Busalama aliongeza wataanza kwa kuwakamata watoto wote walioko mitaani na wale wanaonekana kuwa katika shughuli mbalimbali na kuwabaina ili wawapelekwa kwao kwa ajili ya kuwakamata wazazi wao.
Alisema kuwa baada ya kuwakamata watawafikisha Mahakamani kwa kutumia Sheria ya Elimu ili waweze kuchukuliwa hatua stahiki kwa ajili ya kutoa funzo kwa wazazi wengine.
Mkuu huyo wa Wilaya alisema kuwa haiwezekani Serikali inatumia fedha nyingi kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure kutoka Shule za Awali hadi Kidato cha Nne kisha kunatokea wazazi wanashindwa kuwapeleka watoto wao shule.
“Baada ya kumalizika mwezi wa pili mimi na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya tutanza kupitia katika maeneo mbalimbali wilayani hapa ili kuwakamata watoto wenye umri wa kuwa shule ambao hawapo…tunatoa muda huo ili kuondoa visingizio kwa baadhi ya wazazi vya kusema kuwa tunatafuta hela za kuwanunulia vifaa vya shule kama vile madaftari” alisema Busalama.
Alisema kuwa watoto wote walioandishwa kuingia shule za msingi na Kidato cha kwanza ni lazima wapo shule ifikapo Machi mosi mwaka huo baada ya hapo zitafuata hatua dhidi ya wazazi.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Kaliua Dkt. John Pima alisema kuwa watoto waliopaswa kuanza darasa la kwanza ni 16,185 wakiwa wavulana 8,113 na wasichana ,8072.
Alisema kuwa kati ya hao ni watoto 13,665 sawa na asilimia 84 ndio wameripoti ikiwa ni wavulana 6,938 na wasichana 6,727.
Dkt. Pima alisema kwa upande wa sekondari waliochaguliwa kujiunga na Kidato ni 3,316 sawa na asilimia 81.4.
Alisema hadi hivi sasa wameripoti 2,519 sawa na 76.3 ikiwa ni wavulana 1,365 na wasichana 1,154.
Hivyo makala WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI
yaani makala yote WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/wazazi-kaliua-kufikishwa-mahakamani.html
0 Response to "WAZAZI KALIUA KUFIKISHWA MAHAKAMANI"
Post a Comment