Loading...

WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE

Loading...
WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE
link : WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE

soma pia


WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE

KUANZISHWA kwa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi ni hatua muafaka katika mazingira ya sasa ambapo kuna ongezeko la maeneo ya uzalishaji hususan viwanda kunakokwenda sambamba na ongezeko la matukio ya athari zinazotokana na ajali, magonjwa ama vifo kutokana na kazi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama amewaambia wabunge wa bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati wa warsha ya kujenga uelewa kwa wabunge kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), mjini Dodoma Februari 3, 2018.

Mhe. Mhagama alisema warsha hiyo ni utekelezaji wa ombi lililotolewa na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kutaka wabunge wajengewe uelewa wa shughuli za Mfuko huo. Akifafanua zaidi Mhe. Waziri alisema Mfuko uliundwa Julai 2015 chini ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 ili kulipa Fidia stahiki kwa mfanyakazi aliyeumia, kupata maradhi au kifo wakati akitekeleza majukumu yake ya kikazi kwa mujibu wa mkataba. 

Alisema, Serikali ilianzisha Mfuko huo kwa lengo la kuhakikisha kuwa wafanyakazi wanapata Mafao bora ya Fidia tofauti na Sheria ya zamani ya Fidia kwa Wafanyakazi ambayo viwango vyake vya Mafao ya Fidia vilikuwa vya chini mno. “Mathalan viwango vya juu vya Fidia kwa Mfanyakazi aliyepata ajali kazini ilikuwa ni shilingi 108,000/= huku Mfanyakazi aliyefariki katika ajali ama ugonjwa kutokana na kazi anayofanya kwa mujibu wa Mkataba wa ajira yake ilikuwa ni shilingi 83,000.” Alibainisha Mhe. Waziri.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu), Mhe. Jenista Mhagama (MB), akizungumza kwenye warsha ya siku moja ya kuwajengea uelewa wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu majukumu ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Msekwa, Bungeni mjini Dodoma Februari 3, 2018. Kulia ni Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Andrew Chenge, na katikati ni Mwenyekiti wa Warsha hiyo, ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamatui ya Bunge ya Katiba na Sheria na Mwenyekiti Mwenza wa Bunge, Mhe. Najma Giga.
Mhe. Najma Giga(katikati), akizungumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo. Kamati ya Bunge ya Katiba na Sheria, iliishauri serikali juu ya umuhimu wa waheshimiwa wabunge kukutana nna wataalamu kutoka WCF ili kuwajengea uelewa wa shughuli za Mfuko. 
Mhe. Andrew Chenge, akizunhgumza kwenye warsha hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), Bw. Masha Mshomba, akitoa mada juu ya uelewa wa jumla kuhusu utekelezaji wa Matakwa ya kifungu cha 5 cha Sheria ya Fidia kwa wafanyakazi, sura 263 marejeo ya mwaka 2015 mjini Dodoma leo Februari 3, 2018.
Baadhi ya waheshimiwa wabunge na viongozi wa WCF wakifuatilia warsha hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE

yaani makala yote WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/waziri-jenista-mhagama-wcf-kufungua.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAZIRI JENISTA MHAGAMA : WCF KUFUNGUA OFISI KWA AWAMU MIKOANI KURAHISISHA UTOAJI HUDUMA ZAKE"

Post a Comment

Loading...