Loading...

WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA

Loading...
WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA
link : WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA

soma pia


WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA



Na Hamza Temba - Kondoa, Dodoma
.....................................................
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla jana tarehe 7 februari, 2018 ametembelea Pori la Akiba Mkungunero katika Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma na kuwataka wananchi wanaozunguka pori hilo kusubiri uamuzi wa Serikali  utakaoshirikisha Wizara yake,  Wizara ya Ardhi na Tamisemi katika kujibu maombi yao ya kutaka kupewa sehemu ya ardhi katika pori hilo kwa ajili ya kuendesha shughuli za kibinadamu.

Dk. Kigwangalla ambaye aliongozana na Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji na Wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya hiyo, alitembelea vijiji vinne vya Ikengwa, Keikei Tangini, Keikei na Kisondoko na kufanya mikutano ya hadhara kwa ajili ya kujiridhisha na  kujifunza juu ya mgogoro uliopo baina ya vijiji hivyo na Pori la Akiba Mkungunero.

"Nimefika hapa leo kujifunza juu ya mgogoro huu, nimejionea hali halisi lakini pia nina maelezo ya wataalamu ambayo yapo kwenye maandishi naomba niende nikayasome, niyatafakari ili niweze kushauriana na wenzangu na mwisho wa siku tuweze kuja na suluhu ya namna ya kuondokana na changamoto ambazo zimekuwepo.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (kushoto) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kijiji cha Ikengwa, Mohammed Tabahi aliyekuwa akimunesha mpaka wa kijiji hicho na Pori la Akiba Mkungunero wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilaya ya Kondoa Mkoani Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa ramani ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji.

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akioneshwa mipaka ya Pori la Akiba Mkungunero na Mrasimu Ramani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa, Peter Nyange (kulia) wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kubaini changamoto za mgogoro wa mipaka kati ya pori hilo na vijiji jirani ili kuzitafutia ufumbuzi wa kudumu ambapo alisema Wizara yake kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na TAMISEMI zitakaa pamoja kutafuta suluhu ya mgogoro huo. Kulia ni Mbunge wa Jimbo la Kondoa Vijijini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Ashatu Kijaji. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla (wa tatu kulia) akiteja jambo na Meneja wa Pori la Akiba Mkungunero, Emannuel Bilaso wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma. 
Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangalla akipokea mabango ya malalamiko kutoka kwa wananchi wa kijiji cha Kisondoko kuhusu Pori la Akiba Mkungunero na vijiji jirani wakati wa ziara yake ya kikazi katika pori hilo jana Wilayani Kondoa Mkoa wa Dodoma. 

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA


Hivyo makala WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA

yaani makala yote WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/wizara-ya-maliasili-ardhi-na-tamisemi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WIZARA YA MALIASILI, ARDHI NA TAMISEMI KUAMUA HATMA YA MGOGORO WA PORI LA AKIBA MKUNGUNERO – DK. KIGWANGALLA"

Post a Comment

Loading...