Loading...
title : WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO
link : WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO
WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO
Wizara ya Maliasili na Utalii ya Tanzania Bara na Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi ya Zanzibar zimeweka mkakati wa pamoja wa kuimarisha ushirikiano wa usimamizi wa maliasili, malikale na kuendeleza utalii kwa maslahi ya pande zote za Muungano.
Hayo yameelezwa na Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi baada ya mkutano wa pamoja wa wizara hizo uliofanyika hivi karibuni katika Chuo cha Taifa cha Utalii Jijini Dar es Salaam.
Mkutano huo wa siku moja uliongozwa pia na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Joseph Meza.
Akifungua Mkutano huo wa siku moja, Maj. Gen. Milanzi alisema pamoja na Wizara hizo kutokuwa za muungano imekuepo haja kubwa ya kukutana kwa ajili kujadili na kuweka mikakati ya pamoja ya kuimarisha sekta ya maliasili na utalii na kukabiliana na changamoto zinazogusa sekta hiyo katika Muungano.
"Tumejadiliana kuona ni namna gani tunaweza kushirikiana kwenye masuala mbalimbali ya biashara ya mazao ya misitu, biashara ya Wanyamapori inayohusiana na mikataba ya CITES na mikataba mingine ya ndani na ya Kimataifa.
"Tumekubaliana pia kuhuisha sheria zinazokinzana katika usimamizi wa sekta tunazozisimamia ili kuepuka migogoro inayoweza kujitokeza katika utekekezaji na hivyo kuathiri Muungano wetu," alisema Maj. Gen. Milanzi.
Hivyo makala WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO
yaani makala yote WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/wizara-zaweka-mkakati-wa-kuimarisha.html
0 Response to "WIZARA ZAWEKA MKAKATI WA KUIMARISHA MUUNGANO"
Post a Comment