Loading...

ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI

Loading...
ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI
link : ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI

soma pia


ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI

Na Ramadhani Juma, Ofisi ya Mkurugenzi .

SERIKALI kupitia Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) imetoa zaidi ya shilingi Bilioni 2.1 kwa ajili ya kukarabati Shule za Sekondari za Bihawana na Dodoma zilizopo Manispaa ya Dodoma ikiwa ni sehemu ya utekezaji wa mpango wa Serikali wa kuzifanyia ukarabati mkubwa Shule kongwe Nchini.

Kati ya Fedha hizo, zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 zitatumika kukarabati Shule ya Sekondari ya Bihawana pekee na zaidi ya Shilingi Milioni 900 zitatumika katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.

Akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa kazi ya ukarabati katika shule hizo jana, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Graceana Shirima alisema kuwa, shughuli ya ukarabati ilitanguliwa na upembuzi yakinifu wa hali halisi ya mahitaji ya ukarabati uliofanywa na mtaalamu mshauri ambaye ni Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST).

“Baada ya upembuzi yakinifu, maeneo ya kipaumbele katika ukarabati kwa awamu hii itahusisha Madarasa, maabara, bwalo na jiko,  vyoo, na mifumo ya umeme, mifumo ya TEHAMA na mifumo na maji safi na maji taka” alisema Shirima.

Alisema  awamu hii ya ukarabati inatarajiwa  kukamilika ndani ya kipindi cha  miezi minne, na awamu nyingine za ukarabati zitatekelezwa kulingana na upatikanaji wa fedha.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Graceana Shirima (wa pili kushoto) akikagua shughuli ya ukarabati katika Shule ya Sekondari ya Dodoma baada ya kuzindua rasmi kazi hiyo. TEA imetoa zaidi ya Shilingi milioni 900 kwa ajili ya ukarabati huo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi na kulia ni Mhandisi Lupakisyo Mwalwiba ambaye ni Meneja Miradi kutoka Chuo cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST)  ambaye ndiyo Mtaalamu Mshauri. 
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TEA Graceana Shirima (kushoto) akikagua maeneo mbalimbali yanayofanyiwa ukarabati katika Shule ya Sekondari ya Bihawana iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma jana mara baada ya kufanya uzinduzi rasmi wa kazi hiyo. TEA imetoa zaidi ya Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuikarabati Shule hiyo.

 Ukarabati ukiendelea katika Shule ya Sekondari ya Dodoma.

HABARI ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI

yaani makala yote ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/02/zaidi-ya-bilioni-21-kukarabati-bihawana.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "ZAIDI YA BILIONI 2.1 KUKARABATI BIHAWANA NA DODOMA SEKONDARI"

Post a Comment

Loading...