Loading...

ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20

Loading...
ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20
link : ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20

soma pia


ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20

Na Karama Kenyunko,Blogu ya jamii

ALIYEKUWA mwanajeshi wa Jeshi la Wananchi Tanzania(JWTZ),Ex MT 66807 na wenzake watatu wamehukumiwa kwenda jela miaka 20 baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na meno ya Tembo yenye thamani ya Sh.198.

Hukumu hiyo imesomwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi  Kasonde.Watuhumiwa wengine waliohukumiwa kifungo hicho ni Bakari na Shafii Muhibu Muhibu.

 Hata hivyo, Mahakama imemuachia huru Asha Hassan Ulaya, aliyekuwa akishtakiwa na wenzake hao baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha mashtaka bila ya kuacha shaka yoyote kuwa naye alihusika kwenye tukio hilo.

Akisoma hukumu hiyo, Hakimu Kasonde amesema upande wa mashtaka kupitia mashahidi wake nane wameweza kuthibitisha mashtaka dhidi ya washtakiwa hao watatu pasipo kuacha shaka yoyote kuwa wametenda kosa.

"Mahakama inawahukumu washtakiwa wote watatu kutumikia kifungo cha miaka 20 jela kila mmoja kwenye shtaka la kwanza na vilevile shtaka la pili miaka 20,"amesema Hakimu Kasonde.Pia Mahakama imeamuru meno ya Tembo yarudishwe kwa Mkurugenzi wa Wanyama pori na gari aina ya Suzuki waliyokamatwa washtakiwa waliyotumia kubebea meno hayo itaifishwe na Serikali.

Katika hati ya mashtaka, inadaiwa, Juni 2, mwaka 2016 huko Mbagala Kibondemaji wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, washtakiwa wote walikamatwa na vipande 10 vya meno ya Tembo.Pia washtakiwa hao walikuwa wanadaiwa kukubali kisafirisha meno hayo ya Tembo yenye thamani ya Sh. milioni 198,mali ya Serikaliya Tanzania.

Washtakiwa hao wanadaiwa kukutwa na nyara hizo za Serikali bila ya kuwa na kibali kutoka kwa Mkurugenzi wa wanyama pori.


Hivyo makala ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20

yaani makala yote ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20 mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/aliyekuwa-mwanajeshi-wenzake-wahukumiwa.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ALIYEKUWA MWANAJESHI, WENZAKE WAHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA 20"

Post a Comment

Loading...