Loading...
title : AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho.
link : AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho.
AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho.
Kikosi cha Azam FC
Na Agness Francis Globu ya jamii.
KLABU Bingwa Afrika Mashariki na kati AzamFc kuvaana na MbaoFC ya Jijini Mwanza baada ya kumalizana na Mwadui FC ambapo wanalambalamba hao walitoka kifua mbele kwa kuifunga timu hiyo bao 1-0 katika uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Timu hizo mbili zitapimana nguvu hapo kesho majira ya saa1 Usiku katika dimba la Uwanja Wa Azam Complex Chamazi.
Ambapo kila timu zina presha ya kutaka kupata ushindi wa kuibuka na Alama 3 ili kuweza kuwa kwenye nafasi nzuri zaidi.
Akizungumza na waandishi Wa Habari
Ofisa Habari AzamFc Jaffary Iddy leo katika ofisi zao Mzizima Jijini Dar es salaam amesema kuwa kikosi tayari kipo kambini na kinaendelea na mazoezi.
"Kikosi kipo kambini kinaendelea na mazoezi yake katika kuelekea kwenye mchezo huo wa aina yake Ambapo kila timu inaitaji ushidi, tunaieshimu Timu ya Mbao iko vizuri na Ina kikosi kizuri lakini na sisi Tumejipanga vema kubakiza Alama 3 Nyumbani"amesema msemaji huyo Jaffary.
Maganga amesema kuwa wataendelea kumkosa mchezaji wao Yakubu Mohammed ambaye alipata majeraha pamoja na Kipa wao namba 1 Razack Abarola.
"Wachezaji Wote wako fiti ila tutaendelea kumkosa mchezaji wetu Yakubu Mohammed aliyepata majeraha katika mchezo wa michuano ya kombe la shirikisho FA Cup ambapo tulicheza na timu ya KMC pamoja na kipa wetu Razack Abarola anaemalizia kutumikia adhabu ya kutoshiriki Mechi tatu" amesema Jaffary Maganga.
Hivyo makala AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho.
yaani makala yote AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/azamfc-kuvaana-na-mbao-fc-kesho.html
0 Response to "AzamFc kuvaana na Mbao FC kesho."
Post a Comment