Loading...

DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru

Loading...
DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru
link : DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru

soma pia


DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru

 
Na Heri Shaaban

MKUU wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amesema anakabiliwa na changamoto ya uhaba wa MAJI katika wilaya hiyo kutokana na idadi kubwa ya wananchi na MAJI yanayozalishwa machache.

Sophia Mjema ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni ya wiki ya maadhimisho ya Maji, ameweka jiwe la msingi la ujenzi wa tanki la kuifadhi MAJI kata ya Kisukuru wilaya ya Ilala lenye ujazo wa Lita 150, 000.

" Halimashauri ya Ilala ndio yenye uhaba mkubwa wa MAJI na changamoto nyingi kutokana na Watu wengi kuhamia na msongamano wa shughuli mbalimbali zinazoendeshwa na wanadamu kila siku " alisema Mjema.


Amesema uwepo wa visima vya MAJI vilivyochimbwa na kuwa na MAJI chumvi yasio faa kwa matumizi ya binadamu kama kata ya Kisukuru na maeneo mengi kuwa na maji chumvi hivyo ni vyema tukabuni mikakati ya kupambana na changamoto hizo.

Aidha amewataka wananchi kuweka utaratibu wa kuchemsha MAJI ya kunywa amoja na kunawa mikono kwa sabuni na MAJI safi na salama pindi watokapo chooni ili kusaidia kuondoa au kupunguza milipuko ya magonjwa ikiwemo kipindupindu katika wilaya hiyo.


Amesema kauli mbiu ya mwaka huu 2018 hifadhi MAJI na mifumo ya kiikolojia kwa maendeleo ya Jamii ni  vyema wananchi tukazingatia ujumbe ili kuleta tija na ufanisi katika kubuni , kupanga , kutekeleza na kuendesha usimamiaji miradi ya Maji.

Kwa upande wake Kaimu muhandisi wa MAJI wa MANISPAA ya Ilala Khery Sultan amesema MRADI huo umetekekezwa na MANISPAA ya Ilala chini ya usimamizi wa  mhandisi wa MAJI wa MANISPAA .

Khery amesema tanki hilo  linahifadhi MAJI Lita za ujazo 150, 000 na litaunganishwa na miundombinu ya mabomba ya DAWASCO yaliopo kata  ya Kisukuru kwa ajili ya kutoa huduma kwani lengo la MRADI kuondoa kero na magonjwa ya mlipuko .

Amesema MRADI huo umegharimu fedha za kitanzania shilingi milioni 113,400,9500 hadi kukamilika kwake..

Naye  Katibu Tawala Msaidizi Huduma za MAJI Mhandisi Elnabeth Kingu kutoka OFISI ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam amesema Wiki ya Maji huazimishwa Duniani kote machi 16 hadi  22 Duniani kote na kauli mbiu inatutaka kulinda vyanzo vya. Maji ambavyo utegemea uwepo wa MAJI, chakula, na nishati .

Kingu amesema katika mkoa wa Dar es Salaam hutegemea MAJI ya ardhini yatokanayo na mzunguko wa MAJI ya mvua (hydrological cicle ),ambapo alisema MAJI hayo yanaitaji ulinzi mkubwa wa Mazingira na endapo yakiathiriwa na uchafuzi wa Mazingira hayawezi kusafishwa.


Hivyo makala DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru

yaani makala yote DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/dc-mjema-azindua-mradi-wa-maji-kisukuru.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DC Mjema azindua mradi wa maji kisukuru"

Post a Comment

Loading...