Loading...
title : HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA
link : HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA
HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA
Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amesema Serikali Mkoani humo haijawakataa wadau wa Afya kutoka katika Mashirika mbalimbali ya Kitaifa na Kimataifa wanaofanya kazi mbalimbali katika kuunga mkono juhudi za Serikali kwenye Sekta ya Afya, bali inatambua mchango wao na inawaomba kufanya kazi kwa kuzingatia vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa kwenye Sekta ya Afya.
Mtaka ameyasema hayo katika mazungumzo maalum na waandishi wa Habari wakati alipokuwa akifafanua kauli aliyoitoa katika kikao kilichofanyika Februari 25 na 26 Mjini Bariadi kati ya Viongozi wa Mkoa huo na Wadau Afya mkoani humo ya kuwataka kuelekeza zaidi fedha zao katika kujibu mahitaji ya wananchi kwenye Afya badala ya semina na mafunzo kwa watumishi.
Amesema Serikali inatambua mchango wa Mashirika na wadau wa Afya Mkoani humo kutokana na mambo waliyoyafanya kuunga mkono Serikali kutatatua changamoto mbalimbali za Sekta ya Afya, ikiwa ni pamoja na kutoa magari, kujenga majengo ya upasuaji katika baadhi ya Vituo vya Afya na kuwajengea uwezo watumishi wa afya.
Ameongeza kuwa pamoja na michango hiyo Mashirika mengi yanayofanya kazi Mkoani Simiyu katika Sekta ya Afya yameonekana kujikita zaidi katika kutoa fedha nyingi kwa ajili ya semina na mafunzo kwa watumishi wa Afya , badala ya kusaidia katika kutatua changamoto ambazo ni vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa pia katika Sekta ya Afya.
Aidha. Mtaka amebainisha kuwa Vipaumbele vya Kitaifa na Mkoa katika Sekta ya Afya ni pamoja na Ujenzi wa Miundombinu ya Afya ambayo ni majengo ya zahanati, vituo vya afya, vyumba vya upasuaji, hospitali), Vifaa pamoja na vifaa tiba, ambapo alieleza kuwa Mkoa huo una upungufu wa Hospitali ya Mkoa, Hospitali mbili za Wilaya, Vituo vya Afya 112 na Zahanati 291.
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) ofisini kwake Machi O2, 2018 Mjini Bariadi.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA
yaani makala yote HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/hatujawakataa-wadau-wa-afya-tunatambua.html
0 Response to "HATUJAWAKATAA WADAU WA AFYA TUNATAMBUA MCHANGO WAO, TUNAOMBA WAZINGATIE VIPAUMBELE VYA KITAIFA-RC MTAKA"
Post a Comment