Loading...

Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu

Loading...
Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu
link : Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu

soma pia


Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu

Na Robert Hokororo, Ofisi ya Mkurugenzi 

Wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga inatarajia kuwa mwenyeji wa Maadhimisho ya Upandaji Miti Kitaifa yatakayoanza Aprili 3,2018 hadi  Aprili 5,2018. 

Katika kilele cha maadhimisho hayo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hamisi Kigwangalla ambapo kauli mbiu ni ‘Tanzania ya Viwanda inawezekana, panda miti kwa maendeleo ya Viwanda’. 

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Zainab Telack wakati akizungumza ofisini kwake ambapo amebainisha kuwa madhimisho hayo yataambatana na shughuli mbalimbali. Miongoni mwa shughuli zinazotarajiwa kufanyika ni pamoja na zoezi la upandaji miti na kuwa kila kaya itakabidhiwa miche kwa ajili ya kuipanda katika maeneo yao na kutakiwa kuitunza. 

Mhe. Telack alisema kuwa lengo la zoezi hilo la upandaji wa miti ni kuifanya Wilaya ya Kishapu kuwa ya kijani kwa kuondoa hali ya jangwa inayoinyemelea. Sanjari na upandaji miti pia madhimisho hayo yataambatana na utoaji wa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi ili kujenga uelewa wa umuhimu wa uhifadhi wa mazingira. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Kishapu, Mhe. Nyabaganga Taraba alisema maandalizi yanaendelea vizuri na kutaja maeneo yatakayopandwa miti ni vijiji vya Mwatuju kata ya Shagigilu na Songwa. Alisema maadhimisho yataambatana pia na maonesho ya bidhaa za misitu pamoja na burudani kutoka kwa wasanii mbalimbali ambapo vyote hivyo vinatarajiwa kuoneshwa katika viwanja vya Shirecu. 

Mhe. Taraba alitumia nafasi hiyo kuwahimiza wananchi kuendelea kupanda miti katika maeneo yao na kuitunza ili kuendelea kuhifadhi mazingira na kuepusha mabadiliko ya tabianchi ikiwemo ukame. 

Tayari Halmashauri ya Wilaya kwa kushirikiana na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) Kishapu wameanza uhamasishaji na utoaji elimu ya uhifadhi wa misitu umeanza kufanyika katika maeneo mbalimbali ya wilaya hiyo ikiwemo utoaji wa elimu kwa njia ya sinema.


Hivyo makala Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu

yaani makala yote Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/maadhimisho-upandaji-miti-kitaifa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Maadhimisho Upandaji Miti Kitaifa kufanyika wilayani Kishapu"

Post a Comment

Loading...