Loading...
title : Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga
link : Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga
Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga
HALI ya taaharuki, leo imetanda katika Mtaa wa Kibasila, Kata ya Upanga Mashariki , Wilayani Ilala, jijini Dar es Salaam, kufuatia kundi la mabaunsa, kuvamia nyumba wanayoishi wanawake tupu na kuwafanyia vitendo vya udhalilishaji.Mabaunsa hao inadawa walitumwa na kanisa moja (jina linahifadhiwa kwa sababu maalumu) ili kuziondoa kinguvu familia nne zinazoishi katika nyumba hizo zilizokuwa mali ya Shirika la Maendeleo Tanzania (NDC).

Inaelezwa, mabaunsa hao walivamia nyumba hiyo majira ya saa 1:30 asubuhi na kukuta baadhi ya wanawake wakiwa wamelala ambapo walivunja milango ya vyumba na kuwadhibiti huku wakiwapekua maungoni wakijifanya kutafuta simu.
Inaelezwa, walipekua katika droo na kupora vitu, fedha na mali za thamani huku wakiwatishia kutokupiga simu mahari popote.

Mabaunsa hao walisomba samani za ndani na kuzitupa umbali wa mita 15 nje ya nyumba hiyo, kuvunja baadhi ya vitu na kumwaga chakula.
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kibasila, Upanga Mashariki, Rukia Liyami, ambaye pia ni anaishi katika nyumba hiyo ameliita tukio hilo ni la kinyama.
Amesema, mabaunsa hao hawakujitambulisha walikotokea na wengi walikuwa wananukia harufu ya pombe.

“Hii nyumba tunaishi wanawake tupu na hawa waliokuja ni wanaume. Wameingia katika vyumba na kutudhalilisha. Huu ni unyama. Tunaomba sheria ichukue mkondo wake,”alisema Rukia.
Amesema, nyumba hizo zilikuwa ni mali ya NDC na , ziliamriwa ziuzwe kwa wakazi waliomo ndani ya nyumba hizo lakini baadaye ziliuzwa kwa kanisa kinyume cha maelekezo hivyo wakazi wa nyumba hiyo kwenda mahakamani mwaka 2008 kupinga nyumba hizo kuuzwa kwa watu ambao si wakazi na kesi bado inaendelea Mahakama ya Rufaa.
“Ni sawa wamekuja kututoa ila serikali ipo, wangetoa barua kwa serikali, Ofisa Mtendaji na Polisi wapo mbona hawakujulishwa?” alihoji Rukia.
Aliongeza; “Kama walitumwa na kanisa basi hii ni dhambi kubwa. Huu ni unyama. Tunalaani vikali. Wameona leo (jana)ni mwisho wa wiki, Jumapili na kuna Jumatatu ya Pasaka hivyo waka chukua kigezo kuwa kutakuwa hakuna kimbilio,”
Aizi Mkindi alisema; “Walipoingia tuliwauliza wanahati zozote za kutoka mamlaka husika? Wakadai wametumwa na kanisa na nyumba ni mali yao.
Tuliwauliza vitambulisho vyao, walikataa kuonyesha na kuanza kututishia maisha,”alisema Mkindi.
Salma Abdalah alisema; “Tulijua tumevamiwa na majambazi. Muonekano wao ulikuwa kama vibaka wazoefu.
Nilijaribu kukimbia walinikamata na kunidhibiti kisha wakaanza kunipora simu yangu ya mkononi.
Nilimpasia mdogo wangu mtoto ili akimbie naye.Niliporejea ndani nilikuta wameingia chumbani kwangu wakipekua na kuiba,”alisema.
Aliongeza; “Katika pochi langu kulikuwa na sh.500,000 na seti mbili za dhahabu ambazo nilipewa kama zawadi yangu ya harusi,”
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa huo, Sadiq Mohammed Ally, aliliita tukio hilo ni la fedheha hivyo kuiomba serikali kuingilia kati.
“Familia nne hazina mahari pa kuishi.Vyombo vimeharibiwa na kutupwa nje,”.alisema.
“Ilitakiwa taarifa itolewe, serikali ya mtaa na mimi mjumbe. Hakuna hati yoyote iliyotolewa kama wametoka mahakamani au mamlaka yoyote. Hatua kali lazima zichukuliwe,”alisema Ally.
Kamanda wa Polisi Mkoa Maalumu wa Kipolisi, Salumu Hamduni, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo.
“Tukio tunalo na bado suala lipo katika uchu nguzi,”alisema Kamanda Hamduni.
Ameongea, sisi polisi tunasimamia amri halali za mahakama, kama kungekuwa na agizo lolote tulilipaswa kultewa taarifa. Ofisi yangu hainataarifa ya amri ya utoaji mali katika nyumba hizo,”
Amesema kama hakukuwa na taarifa basi tukio hilo limefanyika kinyume cha sheria au hawakuona umuhimu wa polisi kushirikishwa.
Hamduni alisema tayari wanamshikilia mtuhumiwa mmoja aliyeshiriki na wanaendelea kumhoji huku msako kwa wahusika wengine ukiendelea.
Hivyo makala Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga
yaani makala yote Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mabaunsa-wawavamia-makazi-ya-wanawake.html
0 Response to "Mabaunsa Wawavamia makazi ya wanawake Upanga"
Post a Comment