Loading...
title : MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA
link : MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA
MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA
Na Mary Gwera, Mahakama
MAHAKIMU wapya wanaotarajia kuanza kazi rasmi ndani ya Mhimili wa Mahakama wametakiwa kufanya kazi kwa kuzingatia sheria na taratibu za Mhimili huo.
Akizungumza na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni katika Ukumbi wa Mahakama Kuu-Dar es Salaam mapema Machi 20, Jaji Kiongozi- Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali amewaasa Waajiriwa hao kufanya kazi kwa maadili na kutojihusisha na vitendo vya rushwa.
“Katika ufanyaji kazi wenu wa Uhakimu, mnatakiwa kuzingatia mambo makuu manne ya msingi ni; Ujuzi wa taratibu na mazoea ya Kimahakama, Uelewa kuhusu Sheria za Msingi ‘Substantive law’ na Sheria za Mwenendo ‘Procedural Law’ kuangalia mazingira ya utoaji haki na kadhalika,” alieleza Mhe. Wambali.
Aidha Jaji Kiongozi pia aliwataka Mahakimu hao pia kufanya kazi kwa kuwaheshimu Wadau wote wanaojumuika nao katika mchakato mzima wa utoaji wa haki, ikiwa ni pamoja na Makarani, Wazee na Baraza na wengineo.
“Heshimuni kila mtu mnayeingia naye Mahakamani, kila mtu ana mchango katika upatikanaji wa haki, na moja ya sifa ya Hakimu ni upole lakini upole sio udhaifu,” alisisitiza Mhe. Jaji Wambali.
Mbali na kuwaasa kufanya kazi kwa kuzingatia maadili, Mhe. Jaji Kiongozi aliwaasa pia Mahakimu hao kutojihusisha na masuala ya siasa katika kazi zao.
Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (wa pili kulia) akiongea na Mahakimu wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo (hawapo pichani) walioripoti katika Ofisi za Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam, wa pili kushoto ni Msajili-Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta, wa kwanza kushoto ni Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania na wa kwanza kulia ni Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha.


Baadhi ya Mahakimu wapya 78 wa Mahakama za Mwanzo (hawapo pichani) walioripoti katika Ofisi za Mahakama Kuu- Kanda ya Dar es Salaam wakimsikiliza Mhe. Jaji Kiongozi katika mkutano huo.

Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Wambali (Katikati), Bw. Edward Nkembo, Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu-Mahakama ya Tanzania (aliyeketi kushoto) na Mtendaji-Mahakama Kuu ya Tanzania, Bw. Leonard Magacha (kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Mahakimu wapya wa Mahakama za Mwanzo walioajiriwa hivi karibuni.
Hivyo makala MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA
yaani makala yote MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mahakimu-wapya-wafundwa.html
0 Response to "MAHAKIMU WAPYA WAFUNDWA"
Post a Comment