Loading...

Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu

Loading...
Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu
link : Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu

soma pia


Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu

NYOTA wa muziki wa singeli nchini, Suleiman Jabir 'Msaga Sumu', amesema anashukuru kwa kupata shoo katika wilaya ya Handeni mkoani Tanga, akisema kuwa anakwenda kwa watu wake wa nguvu kutokana na kufahamu kuwa wanaupenda muziki wake.

Akizungumza kwa furaha kubwa, Msaga Sumu anayetamba katika muziki huo alisema kuwa wilaya la Handeni ni kati ya maeneo yaliyoupaisha muziki wake, simu chache baada ya kuibuka kwenye tasnia hiyo kutokana na watu wengi wakiwamo waendesha bodaboda waliokuwa wameziweka nyimbo zake kwenye vyombo vyao vya usafiri na kuzicheza muda wote.

Alisema hivyo shoo mbili alizopata kwa kuanzia Jumamosi ya Machi 24 asubuhi hadi jioni kwenye uwanja wa Mabatini, Mkata, wilayani Handeni pamoja na ile itakayofanyika usiku katika siku hiyo hiyo kwenye Ukumbi wa Rombo Hotel kwa kushirikiana na bendi ya Twanga Pepeta, ni sehemu ya kwenda kutuliza kiu ya mashabiki wake wa muziki wilayani humo, mkoani Tanga.

"Handeni nitaanza Mkata kwenye uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Machi 24 na baadae nitakuwapo Rombo Hotel, Handeni Mjini, nikiamini ni sehemu nzuri kwangu kutokana na nguvu ya mashabiki wangu kwa namna moja ama nyingine.

" Ni watu wa nguvu kwasababu wanaupenda sana muziki wangu, ukizingatia kuwa mimi msanii hivyo napaswa kufahamu mahala gani nakubalika ili kuhakikisha kuwa nalinda tbamani yao kwangu kama njia ya kuendelea kuniletea mafanikio katika kona ya muziki wa singeli ambao bila kuficha mimi ndio mfalme wao kutokana na uwezo wangu kimuziki,"Alisema Msaga Sumu.

Msaga Sumu anayetamba pia na nyimbo ya Mwanaume Mashine, Shemeji na nyinginezo, alitumia muda huo kuwataka mashabiki wake kuingia kwa wingi kwenye maonyesho mawili ya uzinduzi wa ligi ya Handeni Kwetu Cup Mkata na lile la Rombo Hotel, ili wajionee mambo mapya kutoka kwake.

Ligi ya Handeni Kwetu Cup inaanzishwa na mdau wa michezo Kambi Mbwana, huku ikitarajiwa kuanza kutimua vumbi Machi 24 na kufikia ukingoni mwezi Oktoba mwaka huu, huku ikishirikisha timu mbalimbali za wilaya ya Handeni mkoani Tanga.
Mwisho


Hivyo makala Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu

yaani makala yote Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/msaga-sumu-nakwenda-handeni-kwa-watu-wa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Msaga Sumu: Nakwenda Handeni kwa watu wa nguvu"

Post a Comment

Loading...