Loading...
title : Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
link : Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
Frank Mvungi- MAELEZO, Dodoma
Serikali imesema itaendeleza mapambano ya Vita dhidi ya ugonjwa wa Ukimwi kwa kuongeza kasi katika kuzuia maambukizi mapya ikiwemo kutoa elimu kwa umma.
Akizungumza mjini Dodoma wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge inayoshugulikia Ukimwi na Madawa yakulevya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu mhe. Jenista Mhagama amesema kuwa dhamira ya Serikali baada ya kuanzisha mfuko wa Udhamini wa Kudhibiti Ukimwi (ATF) ni kuhakikisha kuwa mfuko huo unajengewa uwezo ili lengo la kuanzishwa kwake litimie.
"Tayari mfuko umeweza kukusanya bilioni 279 katika kipindi kilichopita na mwaka huu bilioni 3 zimetengwa katika Bajeti na zitaingizwa katika mfuko huu ili uweze kutimiza majukumu yake kwa ufanishi na tumekuwa tukiwashirikisha wadau katika kuchangia na wamekuwa wakituunga mkono na tunaendelea kuwaomba wajitokeze zaidi kuchangia mfuko huu " Alisisitiza Mhagama.
Akifafanua Mhe. Mhagama amesema kuwa tayari mapendekezo kuhusu kuwepo kwa tozo maalum katika kodi yameshawasilishwa katika kamati husika kwa hatua zaidi dhamira ikiwa ni kuujengea mfuko huo uwezo wa kuwa na fedha za kutosha katika kufanikisha vita dhidi ya Ukimwi hapa nchini.
Mkakati mwingine ni ujenzi wa kituo maalum katika eneo la Mererani Mkoani Manyara kitakachosaidia katika mapambano dhidi ya Ukimwi kwa kuwa eneo hilo ni moja ya maeneo yenye mwingiliano mkubwa wa watu kutokana na shughuli za uchimbaji madini.
Hatua nyingine ni kufanya kazi kwa kushirikiana kati ya TACAIDS na Mamlaka ya Kupambana na Dawa za Kulevya ili kuwafikia waathirika wa dawa za kulevya ambao ni moja ya makundi yanayoathika na ugonjwa wa ukimwi kwa mujibu wa tafiti mbalimbali.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana Ajira na Wenye Ulemavu Mhe. Jenista Mhagama akizungumzia mikakati ya Serikali kupambana na janga la Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema Bungeni mjini Dodoma. kushoto ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira mhe. Antony Mavunde.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa yakulevya Mhe. Osca Mukasa (Mb) akisisitiza jambo wakati wa warsha kwa wabunge wa Kamati hiyo kuhusu hali ya Ukimwi hapa nchini iliyofanyika mapema mjini Dodoma.kulia ni Katibu wa Kamati hiyo Happiness Ndalu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko akiwasilisha mada kuhusu hali ya Ukimwi hapa nchini wakati wa warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya mapema Bungeni mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Taifa ya Kudhibi Ukimwi (TACAIDS) Dkt. Leonard Maboko (kulia) akiteta jambo na mmoja wa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ukimwi na Madawa ya Kulevya Mhe. Edward Mwalongo (Mb) mara baada ya warsha kwa wajumbe wa Kamati hiyo mapema mjini Dodoma.
Hivyo makala Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi.
yaani makala yote Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/serikali-wadau-kuendelea-kuzuia.html
0 Response to "Serikali, Wadau Kuendelea Kuzuia Maambukizi mapya ya Virusi vya Ukimwi."
Post a Comment