Loading...
title : STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU
link : STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU
STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU
Na Zainab Nyamka Globu ya Jamii.
STAND United yapunguza spidi ya Simba!Ndio kauli ambayo unaweza kuitumia baada ya vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba kushindwa kufurukuta mbele ya wapiga debe wa Shinyanga Stand United kwa kukubali sare ya goli 3-3 katika mchezo uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Katika mchezo huo uliopigwa ndani ya dimba la Uwanja wa Taifa ulichukua dakika 6 timu ya Simba kuandika goli la kuongoza kupitia kwa beki wake Asante Kwasi aliyemalizia mpira uliotemwa na mlinda mlango wa Stand United.
Dakika ya 23, Laudit Mavugo anashindilia msumari wa pili na kufanya usomeke 2-0 ila matokeo hayo hayakudumu ambapo katika dakika ya 36 mchezaji wa Stand United Tariq anamalizia krosi kwa kichwa na kumimina mpira wavuni na matokeo kuwa 2-1.
Baada ya dakika 5 ikiwa ni dakika ya 41 ya kipindi cha kwanza Stand United walisawazisha kupitia kwa Lulambo na matokei kuwa 2-2 mpaka mapumziko.Kipindi cha pili,kilianza kwa kasi na kila timu kusoma mchezo wa mwenzake ambapo Simba walitangulia kupata goli la 3 dakika ya 61 kupitia kwa Nicolaus Gyan.
Hata hivyo kasi ya wachezaji wa Stand United na dakika 6 baadaye mchezaji wa Stand United raia wa Burundi Bigiriama aliisawazishia timu yake na matokeo kuwa 3-3 mpaka kipyenga cha mwisho.Baada ya matokeo hayo Simba anaendelea kukaa kileleni kwa alama 46 wakifuatiwa na Yanga wenye alama 40 wakiwa wamecheza michezo 19.
Matokeo ya Simba na Stand United yameonekana kuwafurahisha zaidi mashabiki na wapenzi wa Yanga kwani alama za Simba kukaa kileleni zimezidi kupungua.
Hivyo makala STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU
yaani makala yote STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/stand-united-wapunguza-spidi-ya-simba.html
0 Response to "STAND UNITED WAPUNGUZA SPIDI YA SIMBA LIGI KUU"
Post a Comment