Loading...
title : MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA
link : MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA
MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA
Mwambawahabari
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo amekabidhi Ticket kwa mgonjwa Ahamed Albayt na watu wengine wanne watakao msindikiza kwenda Nchini China kwaajili ya kupata matibabu.
Akizungumza na waandishi wa habari Mhe. Makonda amesema mgonjwa huyo ni mmoja wa wagonjwa waliokuwa wanatibiwa katika meli ya wachina iliyotiananga katika badari ya Dar es salaam mwishoni mwa mwakajana na kuonekana anatatizo kubwa la viungo vya mwili wake kutofanya kazi na kuahidi kumpeleka china kwa madaktari walikuwa melini kwa kuahidi kuwa watatibiwa katika Hospital ya Beijing Puhua International huku akijitolea pia kugharamia fedha za Matibabu na Malazi.
RC Makonda alitoa ahadi hiyo wakati wa Zoezi la Upimaji Afya Bure kwenye Meli ya Jeshi la China mwishoni mwa Mwaka Jana baada ya kugundulika Ahmed anahitaji Matibabu Maalum ambayo hayapatikani kokote kule duniani isipokuwa China, jambo lililomfanya RC Makonda kutokwa na Machozi na Kuhaidi Kumpeleka kwenye matibabu kwa gharama yoyote ile Maumivu na Mateso anayopitia kijana huyo.
Ahmed Albaity anasumbuliwa na tatizo la uti wa mgongo baada ya kuanguka na kuvunjika Shingo alipokuwa akiogelea ambapo kwa sindano moja pekee inagharimu Dollars 26,000/= sawa na shillingi million 52.
Amesema Ahmed atasafiri Nchini China Siku ya Jumapili akiongozana na watu watatu wa kumsaidia kumuhudumia ambapo gharama zake ni zaidi ya Shilingi Million 100.
Aidha Makonda amesema Shauku yake ni kugusa maisha ya Mwananchi hata kama ni mmoja atakaekwenda mbele za Mungu na kusema Asante Mungu kwa kutupatia viongozi wetu, ifike mahali tumtumikie Mungu katika nafasi zetu, na katika hilo watu wote watakuwa Sawa na tutawahudumia bila kutarajia chochote kutoka kwao kama sehemu ya utumishi wetu ambapo amewashukuru watu wote waliomchangia na kufanikisha matibabu.
Pamoja na hayo Makonda ametoa wito kwa wananchi wa dini zote kumuombea Ahmed ili aweze kuona na kuendelea na shughuli za ujenzi wa Taifa.
Naye Ahmed Albaity amemshukuru mhe. Makonda kwa moyo wa ukarimu aliouonyesha ambapo ameeleza kuwa ameishi kwa mateso muda mrefu kutokana na kukosa uwezo wa kumudu gharama za matibabu.
Ameongeza kuwa, alipokuwa akiomba watu wamchangie wapo waliokuwa wakimvunja moyo kwa kumwambia hawezi kuona lakini RC Makonda ameonyesha moyo wa kipekee.
Hivyo makala MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA
yaani makala yote MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/mgonjwa-aliye-pooza-kwa-miaka-kumi.html
0 Response to "MGONJWA ALIYE POOZA KWA MIAKA KUMI KUTIBIWA CHINA, MAKONDA ATOA MSAADA"
Post a Comment