Loading...
title : TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU
link : TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU
TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU
Na Humphrey Shao, Globu ya jamii
RAIS wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Warace Karia amesema atasimamia suala la bima kwa wachezaji wanaoshhiriki katika Ligi Kuu pamoja na ligi mbalimbali zinazosimamiwa na shiriki hilo ili wachezaji wapate haki zao kwa haraka pindi wanapopata matatizo wakiwa michezoni kwenye maisha yao ya soka.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam,wakati anafungua mafunzo kwa viongozi wa vilabu mbalimbali nchini kuhusu umuhimu wa bima yaliyoratibiwa na Taasisi ya ISDL kwa kushirikiana na Kampuni ya Bima ya Aliance life Insurance, Karia amesema atahakikisha anasimamia suala hilo ili litekelezeke.
"Lazima niwaambie ukweli kuhusu hili suala la bima, kwa sasa nafuatilia kwa ukaribu sana kwa kuhakikisha kila mchezaji aliyesajiliwa katika klabu ya Ligi Kuu na Shirikisho anapatiwa bima ya maisha ili kumsaidia kupunguza pindi yatakapojitokeza wakiwa uwanjani au baada kumaliza mpira wake,"amesema Karia.
Ameongeza kwa sasa lawama nyingi zinatumwa kwa TFF kuwa wameshindwa kuhudmia wachezaji wa zamani lakini kimsingi wa jambo lenyewe kuondokana na lawama hizo ni kuhakikisha wachezaji kila mmoja anapata bima ya maisha yake."Lengo ni kumsaida katika kujikwamua pindi anapopatwa na matatizo na hasa yanayohus maradhi,"amesisitiza.
Ametumia nafasi hiyo kutoa salamu za rambirambi kwa msiba wa mwanamichezo mkongwe aliyewahi kuichezea Klabu ya Simba Arthur Mambeta ambaye amefariki dunia usiku wa kuamkia jana baada ya kusumbuliwa na maradhi ya saratani kwa muda mrefu..
Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia akizungumza wakati wa uzinduzi wa Semina kwa vilabu mbalimbali vinavyoshiriki Michuano ya Shirikisho nchini.
Mwenyekiti wa ISDL , Dkt Katunzi akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais wa Shirikisho la Soka nchini(TFF),Warace Karia kuzindua Semina kwa ajili ya Vilabu mbalimbali hapa nchini.
Viongozi wa klabu mbalimbali nchini wakifatilia kwa makini hotuba ya Rais wa TFF katika Semina Maalum iliyoandaliwa na ISDL kwa kushirikiana na Aliance Life Insuarance.
Hivyo makala TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU
yaani makala yote TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/tff-yaahidi-kusimamia-upatikaji-wa-bima.html
0 Response to "TFF YAAHIDI KUSIMAMIA UPATIKAJI WA BIMA KWA WACHEZAJI LIGI KUU"
Post a Comment