Loading...

AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED

Loading...
AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED
link : AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED

soma pia


AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED

Na Agness Francis, Globu ya jamii

TIMU ya Azam FC imeendelea kujifua kikamilifu kwa lengo la kuhakikisha wanaibuka na ushindi kwenye mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara dhidi ya Singida United, utakachezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam Jumamosi wiki hii.

Mchezo huo utachezwa saa moja usiku na utakuwa na msisimko wa aina yake hasa kwa kuzingatia timu zote mbili zinakaribiana kwa ponti kwenye msimamo wa ligi.Azam FC ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo ikiwa na pointi 35 wakati Singida United ipo nafasi ya nne ikiwa na alama 34.

Wakati timu hizo zikiwa kwenye nafasi hizo, Simba ndio ipo kileleni kwa kuwa na pointi 45 wakati Yanga inashika nafasi ya pili.Kocha Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche na kiungo Frank Domayo wamesema kuwa wanauhakika wa ushindi kwenye mchezo huo.

Cheche amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa wachezaji wote wako vizuri na wana morali ya mchezo."Tuko vizuri tunaangalia michezo iliyopita, matatizo tuliyokuwa nayo kwenye michezo iliyopita tunajaribu kuyasawazisha yasijirudie katika mchezo ujao."Halafu tunaiangalia Singida jinsi gani ilivyo ina uzuri gani ina udhaifu gani ili tutumie madhaifu yao na mazuri yao tuweze kuyadhibiti,"amesema Cheche na kuongeza 

"Tahadhari lazima tuingie nayo kwani hatutaki kufungwa .Tunataka kushinda."Kiungo Frank Domayo amesema watapambana na kufuata maelekezo ya mwalimu ili kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wa Jumamosi dhidi ya Singida United.

Katika mchezo wa raundi ya kwanza, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1 mchezo uliofanyika uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma, bao la Azam FC ilikifungwa na Paul Peter huku Singida wakitangulia kutupia mchezaji wake Danny Sengimana.


Hivyo makala AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED

yaani makala yote AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/azam-fc-yajihakikishia-kuibuka-kidedea.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "AZAM FC YAJIHAKIKISHIA KUIBUKA KIDEDEA DHIDI YA SINGIDA UNITED"

Post a Comment

Loading...