Loading...
title : VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU.
link : VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU.
VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU.
MWAMBA WA HABARI
NA MWANDISHI WETU, DAR ES SALAAM.
Wakili wa viongozi wa Chadema, Frederick Kihwelo amesema viongozi hao wamefutiwa dhamana kwa kuwa wanapotakiwa kuripoti polisi, baadhi yao hushindwa kutokea.
Pia mbunge wa chama hicho Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa naye ameungwanishwa na viongozi waliowekwa mahabusu
Akizungumza leo Kihwelo amesema Mchungaji Msigwa aliitwa na alipofika polisi naye aliunganishwa na wenzake.
Viongozi hao waliripoti polisi Machi 22, 2018 na kutakiwa kuripoti leo. Siku hiyo Mdee na Matiko hawakuwepo huku Mnyika na Heche wakihojiwa kwa zaidi ya saa mbili kutokana na kutoripoti siku za nyuma.
Februari 20, 2018 Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam iliagiza kukamatwa viongozi saba waandamizi wa Chadema, siku chache baada ya tukio la kuuawa kwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Akwilina Akwilini.
Akwilina aliuawa kwa kupigwa risasi Februari 16 akiwa ndani ya daladala eneo la Mkwajuni, Kinondoni wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chadema waliokuwa wakienda ofisi za mkurugenzi wa Halmashauri ya Kinondoni kudai viapo vya mawakala wao.
Hivyo makala VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU.
yaani makala yote VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU. mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/viongozi-chadema-watupwa-mahabusu.html
0 Response to "VIONGOZI CHADEMA WATUPWA MAHABUSU."
Post a Comment