Loading...
title : WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI
link : WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI
WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI

Na Said Mwishehe, Globu ya jamii
KADIRI kengele inavyogonga kuashiria sikukuu ya Pasaka ipo jirani, ndivyo dhahiri kuwa siku za kuelekea Tamasha la Pasaka zinahesabika. Ni Aprili Mosi, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.
Tumezoea mara nyingi kushuhudia Tamasha la Pasaka likifanyika jijini Dar es Salaam lakini waandaaji wa tamasha hilo wameamua mwaka huu iwe zamu ya Kanda ya Ziwa. Hivyo Pasaka hii, watu wa Kanda ya Ziwa watahemewa kwa burudani ya nyimbo zenye kumsifu na kumtukuza Mungu na litanenwa neno la Mungu.
Hivyo Aprili Mosi ni CCM Kirumba, Aprili Pili Tamasha la Pasaka litachukua nafasi kwenye Uwanja wa Halmashauri, mkoani Simiyu. Hakuna ubishi tena katika sikukuu ya Pasaka mwaka huu wakazi wa Kanda ya Ziwa, eneo ambalo litakuwa sahihi kwao kuisheherekea siku hiyo ni kwenye Tamasha la Pasaka.
Wakati siku zikikaribia kuelekea Tamasha la Pasaka kwa mkazi wa Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa jumla ni kuendelea kumuomba Mungu ili aendelee kukupa uzima na afya njema.Waandaaji wa tamasha hilo, Kampuni ya Msama Promotion, mwaka huu wameamua kuweka vionjo tofauti ili kuhakikisha tamasha hilo linafanyika na kuacha historia kwa wakazi wa Kanda ya Ziwa.

Natamani kutaja baadhi ya nyimbo zake atakazoimba siku hiyo lakini acha nikae kimya. Sitaki kukumalizia uhondo. Vema ufike CCM Kirumba kisha Uwanja wa Halmashauri, Simiyu ili macho na masikio yako yapate kumuona na kumsikiliza Rose Mhando. Uwezo wake wa kuimba umemfanya awe nyota ya muziki wa Injili.Kwa Rose Mhando mwenyewe anajua ukubwa wa Tamasha la Pasaka.
Hivyo makala WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI
yaani makala yote WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/waimbaji-mahiri-wa-nyimbo-za-injili.html
0 Response to "WAIMBAJI MAHIRI WA NYIMBO ZA INJILI KUTIKISA KANDA YA ZIWA TAMASHA LA PASAKA APRILI MOSI"
Post a Comment