Loading...

WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA

Loading...
WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA
link : WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA

soma pia


WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu ametoa miezi mitatu kwa wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanatenga asilimia 4 za fedha za halmashauri kwaajili ya kuwapa wanawake mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi na kuunga mkono juhudi za serikali katika uchumi wa viwanda.

Amesema kuwa serikali haitasita kuwawajibisha wakurugenzi watakaokiuka maelekezo ya serikali yanayolenga kutekeleza ahadi za Mheshimiwa Rais kwa wananchi ili kuwawezesha wanawake wa mijini na vijijini kiuchumi na hatimae kujiongezea kipato na kuwezesha uchumi wa viwanda.

“Linapokuja suala la kuwawezesha wanawake kiuchumi hatutanii, chama cha mapinduzi tumepewa kura na wanawake wa Tanzania hasa wanawake wa vijijini na tumewaahidi wanawake kwamba tutawapa mikopo yenye masharti nafuu, kwahiyo pale ambapo mkurugenzi anashindwa kutenga fedha kwaajili ya kuwapatia wanawake mikopo hatutaelewana, na tunasubiri mpaka tarehe 30 June 2018 wakurugenzi wote ambao hawajatenga fedha na kuzitoa kwaajili ya wanawake  tutapeleka majina yao kwa Mh. Rais Dk. John Pombe Magufuli,” Mh. Ummy alisisitiza.

Halikadhalika Mh. Ummy amepiga marufuku suala la kutoa fedha ndogo kwa kikundi kikubwa cha kinamama huku akitolea mfano kikundi cha watu sita kupewa 300,000 kuwa haitawasaidia kinamama hao katika juhudi za kujikwamua kiuchumi na kuongeza kuwa ni heri fedha hizo zikabaki kwa mkurugenzi ili ifanye shughuli nyingine lakini sio kuwakwamua kinamama.

 Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu akiserebuka na wanafunzi wa shule ya sekondari Kizwite katika maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani yaliyofanyika Kimkoa katika manispaa ya Sumbawanga, kushoto kwake niMwakilishi wa Balozi wa Canada. Bi. Susan Steffen pamoja na wanafuinzi. 
 Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu (wa pili toka kushoto)  akiwana  Mwakilishi wa Balozi wa Canada Bi. Susan Steffen (anayemfuatia) na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Dk. Khalfan Haule muda mfupi kabla ya Mh. Ummy kutoa hotuba yake.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto  Mh. Ummy Mwalimu akitoa maelekezo kwa wakurugenzi nchini Tanzania bara juu ya kutenga fedha za mikopo kwa wanawake.
Baadhi ya wanawake walihudhuria kilelelcha siku ya wanawake Duniani yaliyoadhimishwa kimkoa Mjini Sumbawanga Mkoani Rukwa huku mgeni rasmi wa sherehe hizo akiwa Waziri wa Afya Mh. Ummy Mwalimu.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA



Hivyo makala WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA

yaani makala yote WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/wakurugenzi-wasiotenga-fedha-za-mikopo.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "WAKURUGENZI WASIOTENGA FEDHA ZA MIKOPO KWA WANAWAKE KUFIKIA JUNE KUTUMBULIWA"

Post a Comment

Loading...