Loading...
title : Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure
link : Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure
Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure
Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI
Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma wanaosomea Shahada ya Ualimu wameunga mkono jitihada za Serikali ya Awamu ya Tano katika Utoaji wa Elimu Msingi bila malipo kwa kujitolea kwenda kufundisha katika shule za msingi na Sekondari zilizoko katika maeneo yao wakati wa Likizo.
Akizindua mpango huo wa kujitolea kwa wanafunzi walimu zaidi ya 500 Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo amewataka wanafunzi hao kuwa mfano ya kuigwa kwenye shule watakazoenda kufundisha ili kuipa heshima zaidi programu hii iweze kuwavutia walimu wengine zaidi.
Alisema kuwa mnapofika mashuleni mkawe mfano bora kwa wadogo zenu, mkaonyeshe uwezo wenu katika kufundisha na kuwafikishia yale muhimu katika masomo yao, mkaonyeshe Umahiri katika Taaluma yenu ndipo kujitoa kwenu kutaheshimiwa na kuthaminiwa na jamii nzima ya watanzania.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo (aliyesimama) akitoa hotuba yake kabla ya kuzindua programu ya wanafunzi walimu kutoka Chuo Kikuu cHa Dodoma wanaokwenda kujitolea kwenye shule za Sekondari na Msingi zilizo karibu na maeneo wanayoishi.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Dodoma, Pro.Davis Mwamfupe akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kuzindua program ya wanafunzi walimu wa UDOM wanaokwenda kujitolea kwenye Shule za Msingi na Sekondari.
Mratibu wa program ya kujitolea kwa Wanafunzi Walimu Dr. Ombeni Msuya ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma akielelezea namna walivyojipanga kusimamia program hiyo.
Mwenyekiti wa Wanafunzi Walimu wanaokwenda kujitolea akizungumza kwenye uzinduzi wa Programu hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Shule ya Sekondari Umonga iliyopo Mjini Dodoma.
Baadhi ya wanafunzi walimu wa Chuo Kikuu cha Dodoma wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi kabla ya uzinduzi wa program maalumu ya kwenda kujitolea kwenye Shule za msingi na sekondari.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure
yaani makala yote Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/wanafunzi-wa-udom-waunga-mkono-jitihada.html
0 Response to "Wanafunzi wa Udom waunga mkono Jitihada za Elimu Bure"
Post a Comment