Loading...
title : WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI
link : WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI
WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI
WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amewasihi viongozi wa dini nchini wasitumie mahubiri yao kuharibu amani au kuleta mgongano katika jamii.
Pia amesema Serikali inatambua wako watu wanaotaka kuharibu amani iliyopo nchini na ametaka watu hao wasipewe nafasi.
Akizungumza katika mkutano mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (Bakwata) uliofanyika Dodoma,Majaliwa amewasihi viongozi wa dini,mahubiri yao yasiwe chanzo cha uvunjifu wa amani na kufafanua Serikali haitasita kuchukua hatua licha ya kwamba inawajali,kuwathamini na kuwaheshimu viongozi wa dini.
Ameeleza kamwe nyumba za ibada zisiwe kiwanda cha kuzalisha chuki.Kuhusu watu wanaotaka kuharibu amani ya nchi,amefafanua Serikali inatambua wapo watu wa aina hiyo.
"Nawaomba viongozi wa dini kutumia Msahafu na Biblia kuhubiri amani," amesisitiza.Kwa upande wa Waziri wa Nchi ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo amewaomba viongozi wa dini waendelee kusimamia maadili na amani iliyopo nchini.
Awali Muft sheikh Abubakar Zubeir amesema Bakwata inaendelea na kazi ya kuwaunganisha Waislam wa madhehebu yote.
Hivyo makala WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI
yaani makala yote WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/03/waziri-mkuu-ataka-viongozi-wa-dini.html
0 Response to "WAZIRI MKUU ATAKA VIONGOZI WA DINI KUTOHUBIRI CHUKI"
Post a Comment