Loading...
title : CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR
link : CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR
CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR
Na Karama Kenyunko,Globu ya jamii
CHUO cha Maliasili na Utalii jijini Dar es Salaam leo kimewakabidhi vyeti Mama Lishe na madereva taksi 50 baada ya kuhitimu mafunzo ya utalii ikiwa ni muendelezo wa kukuza na kuboresha huduma za utalii nchini.
Akizungumza na wahitimu wa mafunzo hayo yaliyochukua takribani wiki moja katika ukumbi wa chuo hicho Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Jiji Sporah Liana amesema, mafunzi hayo yatakuwa ni muendelezo wa kukuza shughuli za utalii nchini na kuongeza uelewa wa Mama lishe na madereva taksi ambao mara nyingi wamekuwa wakitoa huduma kwa watalii bila elimu ya kutosha
"Tumegundua shughuli za utalii zinafanyika katika kila kona ya Jiji hili, tumegundua pia watallii wanapenda kula chakula kwa Mama lishe kwani ambao wengi wao hawana mafunzo ya kutosha.
"Tunajua wanaofanya kwenye mahoteli makubwa wengi wao wanasoma katika Chuo hiki tofauti na mama lishe ambao hawana mafunzo yoyote, tumeonelea no vizuri na mama lishe pia tuwalete katika mafunzo ili waweza kujua namna ya kutoa huduma kwa watalii wetu" amesema Liana.
Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Sporah Liana akizungumza alipokuwa anafunga mafunzo kwa wajasiriamali ambao ni mama lishe na madereva 50 baada ya kuhitimu mafunzo ya utalii ikiwa ni katika uboreshaji na kukuza huduma za utalii nchini.
Baadhi wahitimu wa mafunzo hayo ya utalii kwa wajasiriamali mama lishe na madereva wa taksi wakisikiliza nasaha za mgeni rasmi
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Chuo cha Utalii Dr Shogo Mlozi Sedoyeka akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na mafunzo hayo ambayo yatawasaidia wajasiriamali hao katika kutoa huduma zenye viwango na kuongeza thamani ya huduma zao.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR
yaani makala yote CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/chuo-cha-utalii-chawatunuku-vyeti-mama.html
0 Response to "CHUO CHA UTALII CHAWATUNUKU VYETI MAMA LISHE, MADEREVA TAKSI 50 DAR"
Post a Comment