Loading...
title : CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi
link : CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi
CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi
Benki ya CRDB leo imetangaza kuanza rasmi kwa kampeni ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiaji wa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa alisema kuwa Benki ya CRDB imeanzisha kapeni hii ili kutoa fursa kwa wateja wake kujishindia safari ya kwenda Urusi kushuhudia fainali za Kombe la Dunia, zinajotarajiwa kuanza mwezi Juni mwaka huu.
“Wateja wetu wenye TemboCardVisa, TemboCardVisa-Electron, TemboCard Visa- Gold, TemboCardVisa-Platinum na TemboCardVisa-Infinite, wakati wa kampeni hii watatakiwa kulipia bidhaa au huduma wanazonunua kwa TemboCardVisa zao kwenye mashine zinazopokea malipo zilizopo sehemu mbalimbali kama migahawa, maduka, mahospitali, vituo vya mafuta na kwingineko ili waweze kujishindia zawadi.
Ili mteja aweze kushinda anatakiwa kufanya miamala mingi zaidi kila wiki. Kadri mteja anavyolipia zaidi kwa kutumia TemboCardVisa yake, ndivyo anavyojiongezea nafasi kubwa zaidi ya kushinda. Washindi wa wawili watakaokuwa wamefanya miamala mingi zaidi kila wiki ndio watajishindia safari hiyo ya kwenda Urusi ambayo itagharamiwa kila kitu na Benki ambapo jumla ya tiketi 24 zitatolewa” alisema
Tully aliendelea kusema kuwa pamoja na washindi wawili wa kwanza kujishindia safari hiyo, Benki pia kila wiki itatangaza washindi wengine 10 ambao watajishindia zawadi kemkem ikiwemo luninga zitakazokuwa zimeunganishwa na kulipiwa kinga’muzi cha DSTV, jezi za timu za mataifa mbalimbali, mipira, kofia, fulana na na zawadi zingine nyingi.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akionyesha vipeperushi vya kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Esther Mwambapa akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati akitangaza kampeni mpya ya Benki hiyo kwa wateja wake, ijulikanayo kama #TwenzetuRussia, itakayowawezesha watumiajiwa kadi za malipo za TemboCard Visa za Benki hiyo kujishindia safari ya kwenda kuangalia mechi za michuano ya kombe la Dunia, zitakazofanyika nchini Urusi kuanzia mwezi Juni mwaka huu.
Hivyo makala CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi
yaani makala yote CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/crdb-bank-kupeleka-wateja-wake-24.html
0 Response to "CRDB Bank kupeleka wateja wake 24 kushuhudia fainali za kombe la Dunia, Urusi"
Post a Comment