Loading...
title : KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA
link : KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA
KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA
Na. Hassan Mabuye, Wizara ya Ardhi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Doroth Mwanyika amewaasa maafisa wapya walioajiriwa katika Wizara yake kuzingatia maadili ya utumishi wa umma wawapo kazini.
Ameyasema hayo wakati alipokutana na watumishi 59 waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
“Suala la huduma bora katika Taasisi za Serikali limekuwa likisisitizwa sana. Sisi kama watumishi wa Serikali ni lazima tutambue wajibu wetu kwa Umma ambao kimsingi ndio waajiri wetu. Wajibu wetu ni kutoa huduma iliyobora na inayokidhi matarajio ya wateja”. Amesema Mwanyika.
Katibu mkuu huo amewaasa watumishi hao kuzingatia Maadili mema ya Utendaji Kazi katika Utumishi wa Umma, kutoa Huduma kwa Mteja na Namna ya kushughulikia Malalamiko, Umuhimu wa Utunzaji wa Kumbukumbu.
Aidha, aliwata watumishi hao kuzingatia mafunzo watakayo pata kuhusu namna ya kujikinga na Janga la Ukimwi na Athari zake, Umuhimu wa Kuwajali Wateja na namna ya Kuwahudumia, Maadili ya Utendaji Bora ikiwa ni pamoja na kujiepusha na rushwa kazini.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bibi. Doroth Mwanyika akiongea na watumishi 59 waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Baadhi ya watumishi waliopata ajira katika Wizara ya Ardhi wakati wakipewa mafunzo ya siku tatu ya kanuni na taratibuza utumishi wa umma yaliyoandaliwa na Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi.
Katibu Mkuu, Doroth Mwanyika akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wapya wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Hivyo makala KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA
yaani makala yote KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/katibu-mkuu-wizara-ya-ardhi-awapa-somo.html
0 Response to "KATIBU MKUU WIZARA YA ARDHI AWAPA SOMO WATUMISHI WAPYA"
Post a Comment