Loading...

MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

Loading...
MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI
link : MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

soma pia


MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

Na Lilian Lundo - MAELEZO, Dodoma
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Dkt. Mwigulu Nchemba amelitaka Jeshi la Polisi kuwaweka ndani madereva wanaosababisha ajali kutokana na mwendo kasi na baadaye kupelekwa Mahakamani.

Dkt. Mwigulu ametoa agizo hilo leo Bungeni Mjini Dodoma alipokuwa akijibu muongozo wa Mbunge wa Ulanga Morogoro Mhe. Goodluck Mlinga, juu ya chanzo cha ajali ya basi la City Boy kutoka Karagwe Mkoani Bukoba kuelekea Dar es Salaam ambalo liligongana uso kwa uso na lori aina ya Fuso lililokuwa linatoka Singida kuelekea Igunga usiku wa Aprili 04 mwaka huu na kusababisha vifo vya watu 12.

"Hatuwezi kuacha watu wanapotea kwa ajili ya uzembe wa mtu mmoja na kuleta hasara na vilio vikubwa kwa Watanzania," alisema Dkt. Mwigulu.

Amesema, ajali nyingi zinazotokea hapa nchini zinasabishwa na mwendokasi na sio tatizo la miundombinu ambapo katika ajali zilizoripotiwa ajali 1500 zilisababishwa na mwendo kasi na ajali 89 zimetokana na miundombinu. 

Aidha Dkt. Mwigulu amesema, Tanzania ni moja ya nchi zenye barabara bora hivyo ajali nyingi zinazotokea husababishwa na uzembe wa madereva pamoja na mwendokasi.

Wakati huohuo bungeni hapo, Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako amesema Serikali imeweka utaratibu mashuleni wa kuwawezesha watoto wa kike kuripoti matukio ya udhalilishaji na pia imeanzisha klabu mbalimbali za kuwajenge uwezo na ujasiri wa kuweza kuripoti matukio ya udhalilishaji.

Hata hivyo Prof. Ndalichako amewataka watoto kutokuwa na uwoga wowote kwa sababu Serikali yao inawalinda, hivyo pale wanapofanyiwa vitendo kinyume na matakwa ya Serikali watoe taarifa ili Serikali ichukue hatua stahiki kwa wale wote wanao wadhalilisha na kusababisha watoto wasisome kwa amani.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba akijibu hoja mbalimbali za wabunge wakati wa Mkutano wa Kumi na Moja wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Mjini Dodoma.


Hivyo makala MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI

yaani makala yote MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/mwigulu-aliagiza-jeshi-la-polisi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "MWIGULU ALIAGIZA JESHI LA POLISI KUWAWEKA NDANI MADEREVA WANAOSABABISHA AJALI"

Post a Comment

Loading...