Loading...

TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

Loading...
TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA - Hallo rafiki SOMA LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala general, makala kisiasa, makala kitamaduni, makala kiuchumi, makala mambo mapya, makala michezo, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA
link : TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

soma pia


TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) imekutana wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kwa ajili ya kupata miongozo ya kufanya kiwanda kiweze kujengwa na kuanza kuzalisha dawa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka hiyo ,Adam Fimbo amesema kuwa kuwakutanisha wadau hao umetokana mkutano wa Mawaziri wa Viwanda , Biashara na uwekezaji pamoja Wizara ya Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia , Wazee na Watoto ambapo TFDA imeona ni muda mwafaka katika kuweza kuwapa muongozo wadau jinsi ya kuweza kuanzisha viwanda hivyo.

Fimbo amesema kuwa TFDA kazi yake kubwa ni kuangalia usalama wa dawa tangu inapozalishwa mpaka inaingia sokoni ikiwa lengo ni kumlinda mlaji na dawa hizo.Aidha amesema kuwa baada ili kiwanda cha dawa kiweze kusajiliwa na kuzalisha dawa hizo lazima vigezo vilivyokwa vizingatiwe.

Fimbo amesema baada ya kupata michoro na kuanza kuzalisha dawa usajili hauzidi siku 15 kutokana na hatua zote zilizofanyika TFDA inakuwa imepitia.
Hata hivyo amesema kuwa hakuna uarasimu wowote katika kusajili dawa au kiwanda nia kumlinda mlaji kwa dawa anazotumia.

“Bila kuwa na usalama wa dawa unaweza ukaua watu ndio maana TFDA tuka kwa ajili ya kazi hiyo ya kuangalia usalama wa dawa za ndani na zinazoingia”amesema Fimbo.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA), Adam Fimbo akizungumza na waandishi habari kuhusiana na kukutana na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa kupata miongozo ya kufanya kuwekeza katika sekta hiyo, leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Mkaguzi wa Viwanda vya Dawa wa TFDA, Proche Patrick akiwapitisha katika miongozo wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa leo jijini Dar es Salaam.
Afisa Msajili wa Dawa wa TFDA, Dk. Shani Maboko akizungumza na wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa jinsi ya usajili wa dawa unavyofanyika katika mamlaka hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wenye nia ya kuwekeza katika viwanda vya dawa wakisikiliza mada zinazotolewa na TFDA . leo jijini Dar es Salaam


Hivyo makala TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA

yaani makala yote TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA mahali kiungo https://somalatest.blogspot.com/2018/04/tfda-yawapa-wadau-miongozo-ya-usajili_5.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TFDA YAWAPA WADAU MIONGOZO YA USAJILI WA VIWANDA"

Post a Comment

Loading...